MASHINDANO ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii inayowahusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (NSSF Media Cup) yameanza kutimua vumbi katika uwanja wa TCC, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Akifungua mashindano hayo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, amewataka wanahabari nchini kuhakikisha wanajiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kujihakikishia maisha ya amani na utulivu baada ya kustaafu.
Alisema kuwa, wanahabari wanapaswa kwenda mbali zaidi katika kulitumia shirika hilo, ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwa wanachama.
Katika ufunguzi huo, timu ya soka ya New Habari (2006) Ltd iliumana na Habari Zanzibar katika Soka, ambako hadi filimbi ya mwisho Habari Zanzibar iliibuka kidedea kwa magoli 4-1, magoli ya Zanzibar yaliwekwa wavuni na Amoor Suleiman aliyeweka wavuni goli moja na Yusuph Juma magoli matatu huku goli la New Habari likiwekwa wavuni na Florian Mwasinde.
Kwa upande wa netiboli, timu ya Jambo Leo iliichapa timu ya Wizara ya Habari Bara kwa jumla ya magoli 59-8, katika pambano la upande mmoja lilipoigwa kwenye viwanja hivyo.
Katika mechi ya pili ya netiboli, Azam Media iliumana na Tanzania Standards Newspaper (TSN), ambako Azam waliibuka washindi kwa magoli 18-13.
Kabaka aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya 11 yanayoshirikisha wafanyakazi wa vyombo vya habari kuonesha ushindani, ufundi na nidhamu ili kuongeza hamasa ya michuani hiyo.
Alivitaka vyombo vya habari kuepuka kuingiza wachezaji wasio wanahabari (mamluki), kudumisha lengo la umoja na ushirikiano baina ya shirika hilo kongwe na vyombo vya habari, ikiwamo kuwapa mazoezi wafanyakazi wa vyombo hivyo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Carolyne Newa wakati alipotemberlea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na mshambuliaji wa timu ya New Habari 2006, Joh Dande wakati wa uzinduzi wa michuano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe Dar es Salaam.
Mchezaji wa New Habari, Jonathan Tito, akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa timu ya Habari Zanzibar, Hamza Hamza katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC, Chang’ombe jijini Dar es Salaam jana. Habari Zanzibar ilishinda 4-1.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo.
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Jambo Leo (kushoto), akimiliki mpira wakati timu hiyo ilipopambana Habari-Maelezo. Jambo leo ilishinda ilishinda 60-8
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Jambo Leo (kushoto), akimiliki mpira wakati timu hiyo ilipopambana Habari-Maelezo. Jambo leo ilishinda ilishinda 60-8
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizundua michuano ya netiboli ya NSSF Media Cup.
Kikosi cha Jambo Leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Azam Media wakati wa ufunguzi wa michuano ya NSSF Media Cup 2014.
Wasanii wa kikundi cha Dar Greater wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment