Sunday, April 6, 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO NYINGINE LONDON UINGEREZA , NA KUPATA MADAKTARI WA KIKE WALIO TAYARI KUJITOLEA KUSAIDIA AFYA YA MWANAMKE TANZANIA KUPITIA WAMA.

Mama Salma Kikwete ametunukiwa Tuzo ya “Global Achievement in Women in Development” na Taasisi ya East Africa Education Foundation iliyoko Nchini Uingereza.
 Tuzo hiyo yenye maana ya “Mafanikio ya Kumuendeleza Mwanamke” ilitolewa wakati Mama Kikwete akiwa Ziarani Uingereza , alipokwenda na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wiki iliyopita kwa Mualiko wa Serikali ya Uingereza .
Akieleza sababu za East Africa Education Foundation kumpatia Mama Salam Tuzo hiyo, Katibu wake Dr.Mohammed Zaharani alisema Taasisi yake imekuwa ikifuatilia kazi za Mama Salma Kikwete kupitia Taasisi yake ya WANAWAKE NA MAENDELEO (WAMA) na kuguswa sana na Kazi anazofanya Mama Salama Kikwete kwa ajili ya kumuendeleza Mwanamke na Mtoto hususan wa kike wa Tanzania.
Katika Hafla hiyo iliyoandaliwa na Chama Cha Wanawake wa KiTanzania Uingereza (TAWA –UK) kwa kushirikiana na Mke wa Balozi wa Uingereza Mama Joyce Kallaghe, kwa ajili ya kumkutanisha Mama Salma Kikwete na Wanawake wa KiTanzania na hususan wale wanaofanya kazi katika sekta ya Afya , kwa lengo la kuazisha Chama Cha Wafanyakazi Wanawake wa KiTanzania katika Sekta ya Afya Uingereza ambao watakuwa wakifanya kazi na WAMA kwa ajili ya kuendeleza afya ya Mwanamke wa Tanzania.
Miongoni mwa Wanawake hawa kuna Madaktari katika Nyanja tofauti , Manesi , Wanamaabara, Walezi , Wakunga n.k . wote ni Wafanya kazi Uingereza. Akiongea na akina mama hao waliojitokeza kwa wingi, Mama Salma Kikwete aliwashukuru sana kwa Nishani waliompatia, kwani alisema inatia moyo kuona kwamba kazi zake zinatambulika.
Vilevile aliwaasa akina mama Kupendana sana kwani mapenzi baian ya wanawake ndio yatakayoleta Umoja wa kweli na kufanya kazi kwa pamoja. Mama Salma pia aliwapa Hamasa akina mama hao kwa kuwaambia wasisite kurudi nyumbani na hata kwenda kugombea katika nafasi kubwa za Uongozi kwani Wanawake wajiamini Wanaweza.
Aliwakumbusha pia akina Mama wa uingereza wliokuwa na furaha sana kwamba ingawa wako nje ya Nchi siku zote wasisahau mila na malezi bora ya watoto, hususan kuzingatia sana malezi ya mtoto wa kike, kwani bila ya kufanya hivyo watoto watapotea na ndio Taifa la kesho.
Licha ya Nishani hiyo aliyotunukiwa Mama Salma Kikwete, pamoja na Ushirikiano ulioanzishwa kwa Madaktari wa kike wa KiTanzania na WAMA , jioni hiyo ilijawa na furaha na shamrashamra nyingi sana kutoka kwa akina mama waliohudhuria kutoka miji mbalimbali ya Uingereza, na walimpa mama yao kipenzi Salma Kikwete Zawadi Mbalimbali kwa furaha ya kumkaribisha Uingereza.



























No comments: