Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi(Burundi) ni Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi. Wa pili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
Kinana akitazama mpaka huo na namna wananchi walivyokuwa wakivuka na wengine kuvushwa kwenye mto wa Malagarasi wakitoka Burundi kuingia Tanzania
Eneo la soko la Murambi, Burundi ambako Watanzania hulazimika kwenda kufanyabiashara na kupata mahitaji huko kutokana na upande wa nchi yao kutokuwa na soko ikiwemo la mifugo lililokuwepo zamani na sasa halipo kutokana na kufungwa kwa sababu zisizojulikana, ambaopo Kinana alihoji kwa nini lisiwepo soko upande wa Tanzania ili kuondoa kero ya watu kuvuka mto kila siku kwenda ng'ambo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa pembezoni mwa mto Malagarasi, mpakani mwa Tanzania na Burundi wakati wa ziara hiyo.
Juu ya maelezo haya ni wananchi wakivuka mto Malagarasi kutoka upande wa Burundi kuingia Tanzania
Baadhi ya wananchi wa Burundi wakiwa wameingia Tanzania baada ya kuvuka mto huo kwa taabu, baadhi yao wameomba serikali za nchi hizo kujenga daraja kwenye mto huo kurahisisha uvukaji
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimlaki Kinana alipowasili kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Buhigwe, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo, leo
Kinana akizungumza na wananchi hao baada ya kumaliza kuzungumza na Kamati hiyo ya siasa. Kulia ni Mbunge wa Buhingwe maarufu kwa jina la Obama
Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Buhigwe wakati wa mkutano huo
Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza ngoma na kikundi cha Kerebuka kilipotumbuiza kwenye mkutano wa Kinana na wananchi wa Buhigwe
Msanii wa kikundi hicho cha Kerebuka kutoka Burundi akionyesha umahiri ake wa kucheza ngoma ya taifa ya nchi hiyo kwenye mkutano huo wa Kinana uliofanyika Buhigwe
Nape akiwa amezungukwa na watoto wa Kijiji cha Kibande, wakati akifanya kazi zake kwenye kompyuta pembeni mwa mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kijiji hicho kata ya Buhigwe
Msafara wa Kinana ukiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na Burundi uliopo Kata ya Munanila, Manyovu wilayani Buhigwe mkaoni Kigoma
Baadhi ya matangazo kwenye mpaka huo
Kinana na msafara wake wakitazama eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi kwenye Kijiji cha Munanila, Tarafa ya manyovu
Vijana wa Kijiji cha Munanila, tarafa ya Manyovu wilayani Buhigwe wakimuonyesha Kinana na msafara wake, uhodari wao wa kucheza ngoma ya Kasimbo ya Kiha, kwenye mkutano uliofanyika Munanila
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Munanila wilayani Buhigwe.
Kinana akiwapungia mikono wananchi baada ya kumfurahisha kwa mapokezi yao, Kijiji cha Munanila alipoowasili kwa ajili ya mkutano wa hadhara
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Kinana, Munanila, Buhigwe
No comments:
Post a Comment