Mhe. Liberata Mulamula akipokewa na mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri mara tu alipowasili kwenye fundraisng dinner ya Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio iliyofanyika Comfort Inn siku ya Jumamosi April 19, 2014.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiingia ukumbini akiwa ameongozana na mweka hazima Bi. Vera Teri.
Mjumbe Michael Mnngodo akiutambulisha uongozi wa Jumuiya kwa Mhe. Balozi Libarata Mulamula na mumewe.
Mjumbe Chiseko Hamisi akielezea mfuko na kazi za mfuko huo na kusisitiza wanajumuiya wajiunge kwa wingi.
Mjumbe Joe Ngwilizi akisoma wasifu wa Balozi Liberata Mulamula.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania wa Ohio kwa kuwashukuru kwa makaribisho mazuri waliyompa na kusisitiza upendo na umoja miongoni mwao pia aliwasifia kwa jitihada zao za kufanya vizuri kwenye maisha kwa kutimiza malengo yao yaliyowaleta huku ughaibuni. Pamoja na kufanya fundraising ya mfuko wa Jumuiya kwa ajili ya kutatua matizo yanayotokea kwenye Jumuiya hiyo, amewaasa kujiandikisha na bima ya WESTADI kwani ni nafuu sana unalipa $300 tu kwa mwaka au kama unaona haiwezekani tafuta bima yeyote hata hapa ughaibuni ili kuondoa adha ya michango michango ambayo wakati mwingine haitimizi malengo na baadae inakuwa usumbufu kwa wengine na alitolea mfano kwa Mtanzania aliyechomwa Wisconsin kwa sio utamaduni wetu tumezoea kuzikwa aidha huku au nyumbani, japo kua hata kuchomwa moto ni gharama pia kwa hiyo ndugu zangu jitahidini muwe na bima. Mhe. Balozi Libarata Mulamula alijibu maswali ya hapo kwa papo na maswali mengi yaligusa swala la uraia pacha kwa Wana Columbus kutaka kujua Ubalozi unasaidiaje swala hilo, Mhe. Balozi aliwajibu kwa kuwaambia swala la uraia pacha ni swala la wanaughaibuni wote lazima kuwa kitu kimoja ili kuweza kufanikisha swala hili Ubalozi kupitia Wizara wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wamelisimia kidedea swala hili lakini kitu kikubwa ni umoja wenu wa kulipa kipaumbele swala zima la uraia pacha.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa katibu wa Jumuiya Bi. Happiness Salukele.
Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri.
Meza kuu kutoka kushoto ni katibu wa jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bwn. Jimmy James.
Watanzania waliohudhuria fundraising dinner.
No comments:
Post a Comment