wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Kajumulo Girls High School wakati wa kusherekea mahafali ya tatu
Wanafunzi wa Kajumulo Girls High School wanaohitimu kidato cha 6 wakati wa kusherekea mahafali ya tatu katika shule yao.
Kwa niaba ya Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea na Mwana hisa wa “VIP Engineering and Marketing Ltd” Mzee James Rugemalira aliyependa kuwa nasi leo lakini akashindwa kutokana na majukumu mengine, tunayo furaha kuwatangazia, kuwa VIP ataanzisha mfuko maalum wa kusaidia katika kuboresha utoaji Elimu katika nchi yetu, utakaoitwa “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust”. Mfuko huu unaanzishwa kwa heshima na kumbukumbu ya mzazi wetu mpendwa marehemu Ma Auleria Kobulungo Muganda.
Mheshimiwa mgeni rasmi, Tunayo furaha kutangaza kwamba shule yetu ya Kajumulo Girls High school ndio itakuwa shule ya kwanza kufaidika na mfuko huu, na leo, VIP kwa niaba ya “Auleria Kobulungo Muganda Memorial Education Foundation Trust” imetoa jumla ya TZS 200 million (TZS 200,000,000) kwa ajili ya kuwasadia baadhi ya watoto wasio na uwezo wa kujilipia lakini wana sifa za kujiunga na kusoma katika shule hii.Baba Methodius Askofu Kilaini nae alitoa neno
Mkuu wa Shule ya Kajumulo Girls High School Jospina Leonidace(kushoto) na kulia ni Fr. Vitus Mrosso (Nyuma) katikati ni Mr. Adrew Kagya akiwa na Rahim Kabyemela
Prof. Anna Tibaijuka akiwa na Mgeni rasmi Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank" kwa furaha wakisikiliza Risala kutoka Wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita
Taswira, Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita wakisoma Risala mbele ya Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe na viongozi mbalimbali Meza kuu.
Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akiteta na Mwl. wa Shule hiyo ya Kajumulo Girls High School
Ni matarajio yetu kuwa mchango huu utawafikia walengwa, wale watoto wenye uwezo na nia ya kusoma, lakini wanatatizwa na karo pamoja na michango mingine ya shule.
Tutashirikiana na Uongozi wa Shule na Wataalam wengine kuweka taratibu za uwazi zitakazoongoza uteuzi wa watoto watakao faidika na msaada wetu. Ninaisihi sana kamati itakayohusika na uchambuzi wa watoto wanaofaa kwa msaada huu itende kazi yake kwa uadilifu ili wale watakaochaguliwa kuhudumiwa wawe wale wanaostahili huduma hii.
Pia, ni matarajio yetu kuwa mchango wetu utakuwa kichocheo kwa watu wengine kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule yetu hii ili iweze kupiga hatua zaidi katika jitihada za kutoa elimu bora kwa mtoto wa kike. Siku hizi watu wengi wanaweka jitihada kubwa kuzungumzia matatizo, wakati wanaweka jitihada kidogo katika juhudi za kuyatatua. Tukishirikiana kwa dhati bila shaka tunaweza kupunguza matatizo ya watoto wetu.
Kwa wale wanafunzi watakaohudumiwa na michango kama hii, ni mategemeo yetu kuwa mchango huu utawaongezea bidii ya kusoma kwa kujiamini bila mashaka kwamba watafukuzwa shule kwa kukosa karo au mahitaji mengine ya shule. Tafadhali weka juhudi ili muweze kusoma vizuri, na mukimaliza shule tuweze kuona matunda ya upendo wetu kwenu. Hakuna tunachodai kwenu, ila mafanikio yenu katika maisha.
Wazazi nao hawakuwa mbali...Wazazi na walezi wa Wanafunzi Kwa Makini Wazazi wakiwaangalia watoto wao huku burudani ya ngoma ikiendelea..Ngoma kutoka Kidato cha kwanza.Watoto wa Kidato cha kwanza wakicheza ngoma huku wakituzwa na Dada zao wanahitimu masomo yao katika shule hiyo ya Kajumulo Girls High School ya Wasichana.Wanafunzi wanaohitimu kidato cha Sita wakiwapongeza wadogo zao kwa kucheza vyema ngoma Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial Bank, Mama Edwina Lupembe akitoa neno.Mr. Andrew Kagya akitoa neno.
Kwanza kabisa ni kudhihirisha kwamba VIP inagawana ndoto (VIP shares the same Vision) na mwanzilishi wa shule hii Prof. Anna Tibaijuka, ya kumkomboa mtoto wa kike ili aweze kujitegemea yeye mwenyewe, wale anaowategemea na hatimae kukomboa Taifa zima. Ni imani yetu (Conviction) kwamba njia bora ya kumkomboa mtoto wa kike ni kumpa elimu bora.
Ni njia ya kuwapa fursa watoto ambao hawana uwezo wa kifedha lakini wana sifa zinazotakiwa kupata elimu bora. Ni wakati wa kuwaonesha watoto hawa kwamba pamoja na ubinafsi unaongezeka katika jamii, bado kuna watu wanaowajali na kuwathamini. Watu ambao wako tayari kuona hata wao wanapata fursa ya kufanikiwa katika maisha. Watoto hawa wakitambua vizuri thamani ya mchango huu, wakatambua thamani ya upendo wa Taifa kwao, na hiyo itawajengea moyo wa kuwasaidia wale ambao hawana uwezo wakiwa watu wazima.
Namna nzuri ya kufundisha upendo, ni kuonyesha upendo, na namna nzuri ya kuonyesha upendo ni kwa matendo.Wanafunzi wanaohitimu kidato cha 6 wakitoa burudani yaoRaha ya kuhitimu Shule..Wanafunzi wanaohitimu Shule hiyo ya Kajumulo Girls High School ya Wasichana wakicheza Ngoma yaoFull kufunguka!!Ngoma kutoka Ngote nayo ilianza kutumbuizaNgoma ikichanganywa vilivyo na Wasanii kutoka kundi la Ngote BukobaMizuka imepanda..Chezea Ngote wewe!Mpaka Viongozi, Prof. Anna Tibaijuka, Mgeni rasmi Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe, Mkuu wa Shule nao wakasimama kucheza ngoma hiyo inayovuma vilivyo hapa Bukoba.Ngoma ilichukua nafasi hapa...Viongozi wakaichambua vilivyo!Unauliza Ngoma Bukoba!!??Prof. Anna Tibaijuka akiikubali ngoma hiyo na kuwapa makofi kwa wingi pamoja na Mgeni Rasmi.Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe; Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank” akuishia hapo alitoa Computer kwa Shule hiyo.
Zawadi ya Computer ikipokelewa na uongozi mzima wa Shule hiyo kutoka kwa Mheshimiwa mgeni rasmi, Bi. Edwina Lupembe ambaye ni Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial Bank”.
Uzinduzi wa Jarida la kila mwaka kwa Shule hiyo ulifanta!Zoezi la Kugawa vyeti pia nalo lilifata...Mzazi akipata picha na Mwanae aliyehitimu Mama na Mwana..
No comments:
Post a Comment