Tuesday, March 11, 2014

LUGUMI ENTERPRISES LTD YAKABIDHI PAMPU YA MAJI NA SHILINGI MILIONI 10 KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA WALIMU MAGU SEKONDARI MAGU.

Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kushoto) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi, kukabidhi msaada wa Pump ya maji inayotumia umeme na fedha taslimu shilingi milioni kumi kwa Afisa Elimu Takwimu (W) Sekondari bw. John M. Mangu  katika makabidhiano yaliyofanyika viwanja vya shule ya Sekondari ya Magu.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu wakati wa makabidhiano ya msaada wa pumpu ya maji inayotumia umeme pamoja na fedha taslimu shilingi  milioni kumi kwaajili ya kukamilisha nyumba ya walimu.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kulia) akiwaongoza wanafunzi wa Magu Secondary kushusha vifaa vya pump ya maji inayotumia umeme ikiwa ni sehemu ya msaada alioukabidhi jana kwa shule hiyo.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kulia) akiwaongoza wanafunzi wa Magu Secondary kushusha pump ya maji inayotumia umeme ikiwa ni sehemu ya msaada alioukabidhi jana kwa shule hiyo kutimiza ahadi iliyowekwa mwaka jana kwenye maafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne na Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi.
Hili ni sehemu ya kusanyiko la baadhi ya wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu waliohudhuria makabidhiano hayo. 
Afisa Elimu Takwimu Sekondari Wilaya ya Magu John M.Mangu (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya sekondari Magu Mwl. Geoffrey Mikenze kiasi cha shilingi milioni kumi alichopokea kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe ili kukamilisha ujenzi wa nyumba ya walimu shuleni hapo.
"Msaada wa Fedha tuliopokea ni huu" Mkuu wa Shule ya sekondari Magu Mwl. Geoffrey Mikenze (kulia) akiwa na wanafunzi wake.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na baadhi ya walimu, wakuu wa idara Shule ya sekondari Magu. 
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na Mkuu wa shule na viongozi wa wanafunzi wavulana Shule ya sekondari Magu. 
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na Mkuu wa shule na viongozi wengine wa wanafunzi wavulana Shule ya sekondari Magu. 
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akipata picha ya pamoja na Mkuu wa shule na viongozi wa wanafunzi upade wa wasichana Shule ya sekondari Magu. 
Serikali ya wanafunzi Shule ya sekondari Magu.
Aksante....
MAGU.
KAMPUNI ya  Lugumi Enterprises Ltd & Ran It Solution imedhamilia kumaliza kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Magu baada ya kutoa msaada wa Pampu mpya ya kusukuma maji ili kukabiliana na kumaliza kabisa kero hiyo Wilayani hapa.

Pamoja na msaada huo Kampuni hiyo pia imetoa kiasi cha fedha shilingi milioni 10 tasilimu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la nyumba ya walimu familia mbili (two in one) ambalo lilishindwa kukamilika kutokana na kukosekana fedha jambo ambalo sasa litakamilishwa na fedha zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo iliyo na tawi lake jijini Mwanza.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi Pampu hiyo na kiasi hicho cha fedha katika viwanja vya shule hiyo Mjini Magu jana, Meneja wa Kampuni hiyo Eligod Sangawe  aliyemwakilisha Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi alisema kwamba utekelezaji wa msaada huo unatokana na ombi la wanafunzi na walimu wa shule hiyo wakati wa sherehe za Mahafali ya 24 ya 2013 kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne kwenye risala yao kwa Mgeni rasmi siku hiyo.

Sangawe alisema lengo kubwa ni kuhakikisha ukarabati na miundombinu ya kufikisha maji shuleni hapo inaimarishwa na kuwezesha maji safi na salama yanapatikana ili kuondoa adha ya kero ya muda mrefu iliyopo katika baadhi ya maeneo ya Mji wa Magu ikiwemo Sekondari hiyo jambo ambalo litawapatia fursa wanafunzi takribani 1,100 waliopo shuleni hapo kutumia muda mwingi katika masomo.

“Jitihada hizi zitasisimua mwamko wa jamii na wadau wengine wa elimu kuona kwamba wanayo nafasi ya kuchangia na kusukuma mbele gurudumu la elimu hapa nchini, hivyo sisi Lugumi Enterprises Ltd & Ran It Solution tunayo matumaini kuwa msaada huu utatatua suala la mahitaji ya maji kwa asilimia 75 huku ule wa kompyuta utawasaidia kukimbizanana na mapinduzi ya Teknohama kutoka mfumo wa analojia na kuingia kwenye mfumo wa kidigitali" 

Meneja Sangawe alisema kuwa kutokana na kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekondari hiyo, Kampuni hiyo hapo awali iliweza kusaidia uboreshaji wa Maabara kwa kutoa vifaa ikiwemo Gesi na zana muhimu, kuboresha mfumo wa maji wa maabara shuleni hapo pamoja na  kukabidhi Computer 3 za ofisi ikiwemo moja ya kufundishia masuala ya sayansi na Teknohama.

Naye Mkuu wa Sekondari hiyo Geoffrey Mikenze alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo na Meneja wake kwa kuamua kutoa msaada huo italeta chachu ya mafanikio ya kielimu kwa shule yake.

“Kwenye risala yetu tulieleza kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji safi kwenye shule yetu, ukosefu wa rasilimali fedha kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya walimu yenye vyumba nane ikiwemo, sebule mbili, stoo mbili (Two in One) Kampuni hii imetusaidia kiasi cha shilingi milioni 10 ili kukamilisha wa ujenzi” alisema Mkuu huyo.


Ametoa wito kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na wananchi ambao walipata kusoma katika sekondari hiyo kuiga mfano ulionyeshwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya Lugumi Enterprises Ltd & Ran It Solution katika kusaidia kutatua changamoto nyingine zilizobaki kama upungufu wa vitabu vya kiada na rejea, upungufu wa matundu ya vyoo nane vya wavulana na vitano vya wasichana ili wanafunzi kufaulu vyema na walimu kutoa taaluma bora.

No comments: