
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia)
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula akizungumza na mhudumu wa afya katika wadi ya wazazi Samazi juu ya huduma na mahitaji ya kituo hicho kipya ambacho kinategemewa kuanza kazi siku za hivi karibuni.


Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula katika Wilaya yake kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la samaki la Kirando linalofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa Ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.



Gati linaloendelea kujengwa kwa ajili yakuhudumia soko hilo la samaki la Kirando wilayani Nkasi.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment