Saturday, February 8, 2014

Waziri Mukangara azindua rasmi mashindano maalum shule za sekondari Dar kwa kishindo, Shule 12 kutoka wilaya tatu za mkoa huo kutoana jasho

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akipeana mkono na wachezaji wa shule ya sekondari Turiani wakati wa ufunguzi wa michuano maalum kwa ajili ya shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Akishuhudia tukio hilo wa kwanza kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo ambayo yatatimua vumbi katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wachezaji (hawapo pichani)  wakati wa ufunguzi wa michuano maalum kwa ajili ya shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Wakifuatilia hotuba hiyo fupi ya ufunguzi wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto) ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo  na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Selestin Mwesigwa (wa kwanza kulia) ambayo yatatimua vumbi katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wachezaji (hawapo pichani)  wakati wa ufunguzi wa michuano maalum kwa ajili ya shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Wakifuatilia hotuba hiyo fupi ya ufunguzi kutoka upande wa kushoto ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (katikati) akibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto) wakati mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam zikiendelea. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (katikati) akibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto) wakati mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam zikiendelea. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (wa kwanza kushoto) akimtambulisha kwa wachezaji Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu (katikati) wakati mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam zikiendelea. Kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (kulia) akipeana mkono na Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali Mstaafu Idd Kipingu wakati mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Selestin Mwesigwa. Kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
 Wachezaji wa timu ya sekondari Kawe (wenye jezi nyeupe) wakipambana kumzuia mshambuliaji wa timu ya sekondari Turiani (mwenye jezi nyekundu) ambao ndio wenyeji wakati wa wakati mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara akipiga mpira na kumchambua Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano maalum kwa shule za sekondari mkoa wa Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya Vodacom ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayotimua vumbi kuanzia katika viwanja tofauti vitatu kwa kila wilaya kuanzia tarehe 8 mpaka 23 ya mwezi Februari.
-------------------------
Mashindano maalum yanayozikutanisha shule kumi na mbili za sekondari kutoka wilaya tatu tofauti za mkoa wa Dar es Salaam yamezinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara katika viwanja vya shule ya sekondari ya Turiani.

Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa na ya aina yake yatahusisha shule kumi na mbili za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam kutoka wilaya zake tatu; kwa wilaya ya Kinondoni shule zitakazoshiriki ni Turiani, Mugabe, Kawe na Kiluvya; Ilala ni Benjamini William Mkapa, Mnazi Mmoja, Majani ya Chai na Juhudi; Temeke ni Kibasila, Temeke, Pendamoyo na Mtoni Relini.

Mashindano hayo yanaanza kutimua vumbi kuanzia Februari 8 na kuhitimishwa siku ya tarehe 23 ya mwezi huu. Viwanja vitakavyotumiwa ni vitatu yaani kimoja kutoka kila wailaya ambavyo ni Kibasila (Temeke), Benjamini Mkapa (Ilala) na Turiani (Kinondoni).

Akizungumza wakati wa mashindano hayo mheshimiwa waziri Dk. Fenella Mukangara alibainisha kuwa ni kwa muda mrefu sasa michezo mashuleni imekuwa ni ya kusuasua kitu ambacho kinapelekea vipaji vya wachezaji wachanga kutoonekana.

“Ni muda sasa tangu michezo mashuleni  kama vile UMITASHUMTA kufanyika, kipindi kile michezo ya aina mbali mbali kama vile mpira wa miguu, netiboli, riadha na mingineyo ilikuwa ikiwakutanisha wanafunzi na kuonyesha vipaji vyao. Tunataka kurudisha hayo mashindano kama ilivyokuwa zamani, naamini kwa kushirikiana na wizara husika pamoja na wadau mbali mbali lengo letu tutafanikiwa.” Alisema Dk. Mukangara

Aliongezea kwa kusema mashindano haya yatafungua njia na kurudisha ari ya wanafunzi kupenda michezo na kuwa ni sehemu ya masomo yao. Hatutaki iwe ni nadharia tu kwamba michezo ni muhimu kwa afya ya mwili na akili.

“Kwa kuanza na shule hizi chache za mkoa wa Dar es Salaam tunaamini mashindano yatakuwa ni yenye msisimko na ushindano mkubwa na tunategemea zoezi hili kusambaa mikoa tofauti ya Tanzania. Ningependa kutoa rai kwa shule zilipata fursa ya kushiriki kuitumia nafasi hiyo ipasavyo, nawatakia maandalizi mazuri, mtuonyeshe soka safi na hatimaye kuibuka na ushindi.” Alimalizia mheshimiwa waziri

Mashindano hayo maalum kwa ajili ya shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam yamedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ambapo walitoa vifaa kama vile jezi, mipira na gharama za uendeshaji kwa kila timu pamoja na kikombe kwa timu itakayoibuka mshindi.

Kwa upande wake akizungumza wakati wa ufunguzi huo Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salum Mwalim amesema kwa upande wao michezo ni kitu muhimu katika jamii yetu na inapendwa na kila mtu hivyo ni jambo jema kuunga mkono jitihada hizo.

“Kampuni ya Vodacom imekuwa ni mdau mkubwa wa michezo nchini na tunashirikiana bega kwa bega na serikali kuhakikisha sekta hiyo muhimu inakua nchini. Kampuni ndiye mdhamini wa ligi kuu Tanzania bara kwa muda mrefu sasa hivyo sasa tunataka tuanzie kuibua vipaji huku ngazi za chini kabisa ili kuja kupata wachezaji bora wataoipeperusha vema bendera ya taifa letu.” Alimalizia Bw. Mwalim

No comments: