Tuesday, February 18, 2014

Tovuti yazinduliwa kurahisisha urasimishaji biashara kwa wazawa

 Dr Ellen Otaru Okoedion Private Sector Development Programme 2013 Team leader from Tanzania, takes participants through a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- launch in Dar es Salaam to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. 
 Dr Ellen Otaru Okoedion Private Sector Development Programme 2013 Team leader from Tanzania, introducing her teammates who also participated in the launch of a new website-www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The ceremony was held in Dar es Salaam at the weekend. 
 Malena Rosman, Head of Development Cooperation Division in the embassy of Sweden (holding a flower boutique and wearing a red jacket) in a group photo with Private Sector Development (PSD) Programme 2013 Team shortly after their graduation and launch of a website to  help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. Far left is Julia Norinder and far right is Daniel Stendahl PSD Programme Tutors.
 Daniel Stendahl (right) Private Sector Development (PSD) Programme Tutor says a word of thanks after being awarded by the 2013 PSD team who graduated in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. Left is Julia Norinder also a PSD programme tutor.
 Julia Norinder (second left) and Daniel Stendahl, Private Sector Development (PSD) Programme Tutors being awarded by the 2013 PSD team who graduated in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. 

Julia Norinder (second left) and Daniel Stendahl, Private Sector Development  (PSD) Programme Tutors being awarded by the 2013 PSD team who graduated in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. 

 Private Sector Development (PSD) Programme Country focal point, Emmanuel Nnko shows one of his gifts he received from Tanzania 2013 Private Sector Development team.
 Private Sector Development (PSD) Programme Country focal points, Saada Mufuruki (left) and Emmanuel Nnko (second right) being awarded by the 2013 Private Sector Development team
 Seasoned entrepreneur Zuhura Muro being awarded by the Tanzania 2013 Private Sector Development team.
 Julia Norinder (second left) Private Sector Development (PSD) Programme Tutor speaks to guests and participants during the launch of a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- introduced to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses.
 Ezamo Maponde, Assistant Director, Private Sector Development in the Prime Minister's office (left) speaks during the launch of a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The website was a brainchild of Private Sector Development (PSD) Programme 2013 Team from Tanzania. Right standing is Daniel Stendahl PSD Programme Tutor and seating is seasoned entrepreneur Zuhura Muro .
Ezamo Maponde, Assistant Director, Private Sector Development in the Prime  Minister's office (right) speaks during the launch of a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The website was a brainchild of Private Sector Development (PSD) Programme 2013 Team from Tanzania. Left is seasoned entrepreneur Zuhura Muro
=======  =======  ========

WAJASIRIAMALI wazawa sasa wanaweza kurasimisha biashara zao kwa urahisi, ziwe ndogo au kubwa, baada ya kuanzishwa kwa tovuti iliyosheheni taratibu zakufuata pamoja na hati muhimu za kisheria zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambazo ujazwa kabla ya kurasimisha biashara.

Tovuti hiyo - www.fanyabiasharatanzania.com – ni zao la Timu ya  Tanzania ya mwaka 2013 katika Programu ya Maendeleo ya Sekta Binafsi iliyopewa mafunzo na Serikali ya Sweden kupitia shirika lake la Sida, ikishirikiana na SIPU International na Jarskog Konsult kwenye masuala ya Mkakati wa Usimamizi wa Biashara na ukuaji wa sekta binafsi.

Akizungumza wakati wa mahafali na uzinduzi wa tovuti hiyo, Kiongozi wa timu, Dk Ellen Otaru Okoedion alisema tovuti hiyo imetengenezwa na timu ya wajasiriamali wakitanzania na wawakilishi kutoka sekta ya umma chini ya mpango wa PSD, unaolenga kuwasaidia wajasiriamali wazawa na watu wengine wanaojihusisha na biashara kupata taarifa mbali mbali muhimu zakuendeleza biashara zao.

"Hii tovuti itawaokolea muda wao, fedha na nguvu zao katika kutafuta taarifa ambazo mara nyingi utawanyika, na kutopatikana kwa urahisi na mara nyingi mjasiriamali ulazimika kutumia gharama kubwa kukusanya taarifa hizi," alisema.

Uanzishwaji wa tovuti hiyo ni hatua ya kuhamasisha ukuaji wa biashara ndogo, wakati huo huo kuunga mkono jitihada za serikali katika kurasimisha biashara hizo, ambazo uhamasisha si tu biashara kuwa na ushindani ndani ya nchi, kanda na kimataifa, lakini pia kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi.

Tovuti hiyo ina taarifa zote muhimu zinazohitajika kuanza, kusajili na kupanua biashara nchini Tanzania.Pia imeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa wizara zote muhimu, mashirika na  sekta binafsi. Pia imetoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za usajili wa biashara zinatolewa na wakala wa usajili wa biashara na utoaji leseni (BRELA).

"Fomu muhimu zakujaza imetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha raia yeyote kuwa na uwezo wa kuelewa na kujaza taarifa zinazohitajika kwa urahisi," alisema Dk Ellen Okoedion.

Alisema kuwa ili kuwafikia watanzania wote, waandaji wa tovuti hiyo wapo mbiyoni kuiunganisha na huduma za simu za mikononi ili kumwezesha hata wale waliopo vijijini kuweza kufurahia huduma hiyo.
"Tovuti hii ni rahisi kuitumia, ikiwa na taarifa juu ya masuala ya biashara, fursa mbali mbali, kama vile mafunzo ya kutosha, zabuni na maonyesho ya biashara," alisema kiongozi huyo wa timu.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi, Ezamo Maponde, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Sekta Binafsi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kuwa ili kufikia ukuaji wa uchumi, mchanganyiko wa uwekezaji katika makampuni mbali mbali ya biashara, rasilimali watu wenye ujuzi, miundombinu bora, mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji wa kigeni vinahitajika.

“Mafunzo haya yamekuwa na manufaa makubwa na mafanikio katika kukabiliana na changamoto za maendeleo yetu, ikiwa ni pamoja na haja ya kupata ukuaji mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi nchini na kupunguza umaskini kwa ujumla," alisema.

Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania ambao wana nia ya kuingia katika ujasiriamali kubadili mawazo yao na kuona ni kama chanzo cha ajira na si kama ajira ya muda mfupi na kuipongeza Serikali ya Sweden kwa kazi nzuri wanayofanya katika kubadilisha na kuboresha sekta binafsi nchini.

No comments: