Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka , akizumgumza na Waandishi wa Habari mjini Morogoro kutoa pongezi na kumshukuru Waziri Membe .
Na John Nditi, Morogoro
RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka amemshukuru Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwa kuanzisha diplomasia ya michezo na nchi za nje pamoja na kufadhili maandalizi ya wanariadha 40 na makocha sita.
Wanamichezo na makocha hao wanapelekwa nje kwa ajili ya kujinoa ili kuwa tayari kwa ajili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Julai 23 hadi Agosti 3, mwaka huu , Glasgow , Scotland.
Rais huyo wa RT alimshukuru Waziri Membe, alipozungumza na waandishi wa habari Mjini Morogoro , Februari 21, 2014 na kusema kitendo cha kuanzisha diplomasia ya mchezo na nchi za nje kimetoa majawabu kwa wanamichezo na viongozi wa Tanzania wanalodeni la kurejea na medali za kutosha kutoka kwenye mashindano hayo.
Kwa mujibu wa Rais wa RT, Wanariadha 20 kati ya hao watakuwa kwenye kambi nchini China , 10 nchini Ethiopia , wengine 10 watakuwa chini Uturuki huku kila kambi ikiwa na makocha wawili .
Hata hivyo alisema wengine wawili wanaenda nchini Kenya ambao watakuwa bila makocha , wakati wanariadha wengine 35 wataendelea na maandalizi nchini hapa kwenye kambi ya mkoa wa Dodoma na Manyara.
Rais huyo wa RT alisema, wanamichezo hao wengi wanatoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Polisi , pamoja na Taasisi nyingie za umma na baadhi wa sekta binafsi iayojitegemea.
Hivyo alisisitiza kwa kusema kuwa, wanamichezo watakaokuwepo katika nchi hizo wakinolewa , watapimwa kutokana na juhudi zao kwenye mazoezi na mafunzo ya michezo watakayoshiriki na wale watakaokidhi viwango vinavyokubalika katika mashindano hayo ndiyo watakaochanguliwa kwenda katika michezo hiyo ya Jumuiya ya Madola.
Pamoja na hayo alisema wanamichezo hao wataedelea kufanya mazoezi katika nchi hizo hadi wakati wa kukaribia kuanza kwa Mshindano ya Jumuiya ya Madola na wale ambao watachanguliwa kulingana na viwango vyao vinavyokidhi wataondokea kwenye nchi hizo kwenda mashindanoni
“ Lazima wanamichezo waitumia fursa hii kuiletea heshima Tanzania katika mashindano ya Madola...historia inaonesha kuwa , wanamichezo wanapopelekwa nje kuweka kambi ya muda kwa ajili ya kufanya mazoezi , wanaposhiriki mashindano haya wanafaya vyema na kurudi na medali nyingi “ alisema Rais wa RT.
Pamoja na hayo alisema “ Shirikisho ya Riadha , wachezaji na viongozi wengine wa Serikali na wananchi kwa ujumla watakuwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema ili kulipa fadhira ya diplomasia ya michezo iliyoanzishwa na Wizara yetu ya Mambo ya Nje chini ya Waziri Membe” alisema Mkata.
Hivyo kutokana na fursa hiyo ametumia fursa hiyo kuwataka wachezaji wote waliochanguliwa kwenda katika nchi hizo kujibidiisha na mazoezi hayo ili wakakidhi matarajio ya watanzania waliokuwa na hamu ya muda mrefu kuiona Tanzania inakusanya medali za kutosha.
Taifa.
Pia amewaomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono juhudi za Serikili ya kuendeleza michezo kwa kutoa misaada ili kuwawezesha wachezaji kuwa na morali ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali ya riadha yakiwemo hayo ya Madola.
“ Serikali imeonesha njia ya kuweka mazingira mazuri ya michezo nchini, awamu ya kwanza ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere iliweka mkazo michezo katika mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali na shule za Masingi, Sekondari na Vyuo tuliyaona matunda yake” alisema na kuongeza.
“ ...Serikali ya awamu ya tatu imetujengea uwanja wa Kisasa ambao pia unakidhi vya kimataifa na katika michezo ya riadha na Serikali ya awamu ya nne umewezesha kuwekeza kwa kuwaleta makocha wa nje wa michezo ya soka, netiboli, riadha , na kujenga misingi imara ya kuinua michezo nchini ” alisema Rais wa RT.
Hata hivyo alisema, michezo ambayo wachezaji watakwenda kunolewa zaidi na ambayo inashindaiwa kwenye mashindano ya jumuiya ya madola ni pamoja mbio fupi, mbio za kati na mbio ndefu , miruko na mitupo.
No comments:
Post a Comment