Tuesday, February 11, 2014

NHC kujenga Satelite City Jijini Arusha

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.

Eneo hilo la Tengeru ambalo zamani lilikuwa likimilikiwa na Hortculture Tanzania Ltd linatazamiwa kujengwa mji wa kisasa utakaojulikana kama Satelite City.

Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa NHC Nehemea Mchechu aliwaambia wajumbe wa kamati ya ardhi ,amaliasili na mazingira kuwa tayari NHC imenunua ekari 600 ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 5.

Nyumba 300 zinatarajiwa kujengwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo kadharika kutajengwa maduka makubwa ,shule pamoja na vituo kwa ajili ya huduma kwa jamii na kwamba ujenzi wa nyumba nyingine 300 utafuati.

Mchechu alisema ujenzi huo hauta athili kwa namna yoyete ile uoto wa asili ikiwemo miti katika eneo hilo na kwamba wanataegemea kuacha sehemu ya Mikahawa iliyopo hapo kama kumbukumbu.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akisalimiana na mbunge wa jimbo la Arumeru Joshua Nassar wakati kamati ya bunge ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akiteta jambo na mkurugenzi wa shirika la hifadhi la taifa(TANAPA)Allan Kijazi alipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City eneo la Tengeru Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akitoa burudani ya nyimbo kwa wajumbe wa kamati ya Ardhi,maliasili na mazingira ilipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City eneo la Tengeru Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akitunzwa na Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya wakati mkurugenzoi huyo alipokuwa akitoa burudani ya Nyimbo ya Bob Marley.
Wajumbe wengine walishindwa kujizuia wakaamua na wao kuonesha vipaji vyao.

1 comment:

Anonymous said...

Kazi nzuri Bwana Mchechu, ila Angalia waist line!