Mtoto wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo.
Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza.
Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.
............................. .............................. .............................. ......
WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la kalenga Iringa zikiendelea kuchukua kasi naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Mwigulu Nchemba amepiga kambi kwa muda Kalenga huku akiibua siri nzito ya Chadema kuanza kununua shahada za wapiga kura.
Mwigulu alisema kuwa kumekuwepo na mbinu chafu inayofanywa na Chadema kwa kuanza kununua shahada za kupigia kura kwa wananchi wa jimbo la Kalenga .
Alisema kuwa Chadema wameanza mbinu hiyo chafu baada ya kubaini wazi kuwa mgombea wa CCM Godfrey Mgimwa tayari amekwisha shida katika uchaguzi huo kutokana na imani kubwa ya wana kalenga kwa CCM.
Hivyo aliwataka wananchi kutodanganyika na pesa zinazotolewa na Chadema kwa kununua haki yao na badala yake kutunza shahada hizo ili kuzitumia kupiga kura kama sehemu ya haki yao ya Msingi.
"CCM imefanya mambo mengi katika jimbo la Kalenga kama kuboresha miundo mbinu na mambo mbali mbali yakiwemo afya , elimu ....jambo ambalo wananchi bado wana imani kubwa na CCM".
Wakati huo huo Chifu Mkwawa Bw Abdu Mkwawa amekigeuka Chadema kuwa kimedanganya umma kuwa Chifu Mkwawa anakiunga mkono chama hicho.
Mkwawa alisema kuwa Dr Slaa amedangaya umma kuwa yeye anaunga mkono Chadema. Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.
No comments:
Post a Comment