Monday, February 10, 2014

Mkutano mkuu wa Jumuiya za Watanzania Italy













Jumuiya za Watanzania Italy,kwa pamoja walifanya mkutano mkuu wa kihistoria siku ya jumamosi tarehe 8/2/2014.

 Mkutano huo uliofanyika mjini Napoli,ulikuwa na madhumuni matatu makubwa. kwanza kuimarisha mshikamano baina ya Jumuiya za Watanzania nchini Italy, na kuzungumzia kero na matatizo ya Watanzania wanaoishi Italy.Wajumbe walichangia yote yaliyokusanywa katika mikutano na vikao vya awali.

Yote yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi na kufikishwa kunakostahili kwa ufumbuzi wa kudumu.

Jambo kubwa la tatu, Wajumbe waliunda kamati ya pamoja ya diaspora yenye wajumbe kutoka NAPOLI,ROMA,MODENA,GENOVA NA PADOVA. Na kuweka majukumu. Wajumbe pia walimchagua:
 Ndugu Kagutta N.Maulidi  (Mwenyekiti)
 Ndugu Ricky JG.Bondo ( kaimu m/kiti)
Ndugu Andrew Chole Mhela (katibu) 
 Ndugu Mwinyimwaka Sarai (kaimu/katibu),
Ndugu LIlian Luhende (hazina)
Ndugu Abdulrahaman A.Alli (mjumbe)
Ndugu Erasmus Luhoyo (Mjumbe)
Ndugu Livinus Mwereke (Mjumbe)
Ndugu Awadhi Sulaiman (Mjumbe)
Ndugu Judith Joseph  (Mjumbe)
Ndugu Zacharia Madjid Mhessa (Mjumbe)

Wajumbe wa mkutano wamependekeza kuwa baada ya kipindi cha miaka miwili  utafanyika mkutano wa kutathmini utendaji wa kamati kwa  ujumla.
Mwisho mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy mh Abdulrahaman A.Alli aliwapongeza baadhi ya viongozi na wajumbe kwa kuwatunukia shahada za uongozi bora na uhadilifu.

No comments: