Monday, February 3, 2014

Mamia wamzika Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar

DSC_0133
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kinondoni kwa ajili ya ibada maalum.
DSC_0140
DSC_0143
Marafiki wa karibu wa familia ya marehemu wakiwa wamesimama kuupoke mwili wa marehemu Meja Mstaafu Isaac Chekingo ulipowasili nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa Juma.
DSC_0047
Mtoto mkubwa wa marehemu (mwenye koti la suti jeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya wanakamati wa msiba ulioongozwa na Afande Thomas Ndonde wa JWTZ.
DSC_0041
Baadhi ya waombolezaji wakitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo.
DSC_0190
Baadhi ya watoto wa marehemu na wake zao wakiwa kwenye majonzi mazito.
DSC_0069
Mtoto mkubwa wa marehemu  Samson Samwel Chekingo (mwenye miwani) akijadiliana jambo na wadogo zake kabla kuanza kwa misa ya kumwombea marehemu baba yao.
DSC_0228
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
DSC_0245
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha (katikati) akiwa amejumuika na baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
DSC_0086
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamefurika nyumbani kwa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
DSC_0263
Mchungaji Charles Mzinga kutoka Kanisa la Usharika wa Azania Front akiendesha ibada ya misa ya kumwombea marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa juma.
DSC_0291
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha akijumuika na waombolezaji wengine kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
DSC_0388
Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
DSC_0452
Pichani juu na chini ni watoto wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo wakitoa heshima za mwisho kabla ya kuelekea makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi.
DSC_0457
DSC_0463
Vilio na simanzi vilitawala.
DSC_0485
Mke wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa mume wake.
DSC_0568
Pichani juu na chini Familia ya marehemu ikiwa katika makaburi ya Kinondoni tayari kuanza shughuli za mazishi.
DSC_0572
DSC_0583
Mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo ukiwasilia katika makaburi ya Kinondoni huku ukiwa umebebwa na Askari wa JWTZ.
DSC_0591
DSC_0641
Mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo ukiteremshwa kaburini.
DSC_0686
Askari wa JWTZ wakitoa heshima za mwisho kwa kupiga risasi hewani kwa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
DSC_0672
Baadhi ya askari wa JWTZ wakitoa heshima wakati mirindimo ya risasi ikilia hewani kwenye mazishi ya Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
DSC_0649
Baadhi ya watoto wa marehemu wakimlilia baba yao.
DSC_0716
Mke wa  marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume wake.
DSC_0722
Pichani juu na chini ni ndugu wa karibu wa marehemu wakiweka mashada ya maua.
DSC_0724
DSC_0724
DSC_0727
DSC_0744
DSC_0760
Kaka wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi la mdogo wake.
DSC_0764
Mratibu wa shughuli ya mazishi ya Meja Mstaafu Samwel Chekingo, Afande Thomas Ndonde wa JWTZ akiweka shada la maua kwenye kaburi.
DSC_0766
Afande Thomas Ndonde wa JWTZ akitoa heshima kwenye kaburi la Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
DSC_0740
Wawakilishi kutoka shirika la Ndege la Air Tanzania alipokuwa akifanya kazi marehemu mpaka mauti yanamkuta, wakiweka shada la maua.
DSC_0769
Ndugu wa karibu wa Marehemu Bw. Zecharia Hans Poppe akisoma wasifu wa marehemu Meja Mstaafu Samuel Chekingo. Picha zote na Mo Blog

No comments: