Katibu Tawala Mkoa wa Katavi akimwongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mama Anna Maembe wakati akikagua eneo la chuo cha maendeleo Msaginya wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo anaye mfuatia kushoto kwa Katibu Mkuu ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Nsimbo Alex Magesa Na Mwisho mwenye SUTI YA kijivu ni Mkuu wa Chuo Msaginya Peter Kikunda ambaye ni mwenyeji akiwatembeza wageni.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mama Anne Maembe akipatiwa maelezo kuhusu bweni la wananchi wa kike liliezuliwa na upepo kufuatia mvua mwaka jana hali iliyofanya kusimama kwa masomo katika chuo hicho kutokana na ukosefu wa mahali pa kulala kwa wanafunzi wa Kike.
Baadhi ya majengo ya chuo Msaginya yanaonekana kuchaka kutokana na kukosa ukarabati kwa muda mrefu hali inayoonesha chuo kama vile kimesahaulika ambacho kinamilikiwa na wizara ya maendeleo ya jamii,lakini ni mali ya wananchi ingawa hawaoni umuhimu wa kuwa na chuo hicho,juhudi za makusudi zinahitajika na ubunifu zaidi ili kunusuru chuo hicho.
Na Kibada Ernest- Katavi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Anna Maembe ameshauri watendaji wa Wizara hiyo kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi za kila siku kwenye maeneo yao ili kuleta mabadiliko katika jamii wanayoitumikia katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Mkuu alitoa kauli hiyo mkoani Katavi alipokutembelea mkoa huo na kukutana na watendaji wa Wizara yake na kupata nafasi ya kukitembelea Chuo cha Maendeleo ya wananchi Msaginya kilichoko Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mlele ambacho kinakabiliwa na changamoto kibao hali iliyosababisha kushindwa kusajiri wanachuo wa kujiunga katika fani mbalmbali mwaka huu wa masomo.
Mbali ya kukitembelea Chuo hicho pia alipata nafasi ya kukutana na vikundi vya vya kinamama waliojiunga pamoja kw a ajili ya kupata na mikopo wanayowezeshwa na Halmashauri kutokana na fedha za ndani ili kuwajengea uwezo akimama waweze kuondokana na utegemezi kwa kuanzisha baiashara ndogondogo ambazo huwasaidia kujikimu kimaisha katika familia zao kama kusomesha watoto,matibabu na huduma nyingine za kijamii.
Pamoja na kukutana na vikundi vya uzalishaji mali kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa huo za Wilaya Mpanda,Halmashauri ya Nsimbo,pamoja na ile ya Mji wa Mpanda kupokea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo akinamama hao, pia alipata nafasi ya kukutana wakurugenzi wa Halmashauri hizo na wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na wafanyakazi wa Idara hizo akapokea changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi na namna ya kukabiliana nazo.
Awali akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi alipokea Taarifa ya Mkoa kuhusu utekelezaji wa kazi za Idara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto iliyotolewa na Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Emmanuel Kalobelo kwa kueleza namna Mkoa ulivyojpanga kukabiliana na changamoto zilizopo najinsi wanavyosaidia kuwawezesha wananachi kuondokana na umasikini hasa kupitia Halmashauri zimejipanga kuwezesha kwa kuunda vikundi vya akinamama pamoja na vijana kuwawezesha kujiaajili kwa kutumia rasilimali zilizoko kwenye maeneo yao.
Akiongea katika kikao hicho Mhandisi Kalobelo alimweleza jinsi Mkoa kupitia kwenye Halmashauri zinavyotekeleza utendaji kazi kwa kuwaunganisha wananchi ili kuwaletea maendeleo,kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi kupitia kwenye vikundi vya uzalishaji mali vya akina mama na Vijana kujiunga pamoja na kuwezeshwa mikopo kupitia kwenye Halmashauri.
Akizungumzia kipimo cha utendaji kazi kwa mtu kuwepo kwenye nafasi Fulani aliyoanayoatapimwa na kwa ufanisi wake kuonekena katika nafasi hiyo ameleta mabadiliko gani kutokana na uwepo wake pale ameisaidiaje jamii kutokana na uwepo katika nafasi hiyo.
Alisisitiza kuwa itafika wakati kujitathimini kwa kila mmoja nini amefanya kwa nafasi aliyonayo katika kutekeleza majukumu yake, katika nafasi aliyokabidhiwa katika kuleta mabadiliko yenye tija katika jamii.
Katibu Tawala huyo alieleza kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kuwa mbunifu na kusoma mazingira ya eneo analofanyia kazi atumie rasilimali zilizopo kuweza kuwanufaisha wale anaowatukia awe mbunifu kwa ajili ya maendeleo ya eneo lake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Halmashauri ya Mpanda Estominh Chang’ah alimweleza Katibu Mkuu kuwa Halmashauri ya Mpanda iwejiwekea mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kupitia makundi ya akinamama na VIjana kwa kuwahamasisha kujiunga kwenye vikundi vya uzalishaji mali na kuwawezesha mikopo kutoka kwenye mfuko wa maendeleo jamii kwa kutumia fedha zilizotolewa Halamashuri.
Akizungumzia suala la kukopa amesema menejementi ya ukopaji ya mikopo bado haijaingia ipasavyo miongoni mwa jamii,na mtu akipewa mkopo bado urejeshwaji wake bado uko chini, Halamashauri katika kukabiliana na changamoto hizo imejipanga na kujiwekea mikakati mizuri kuwahamasisha wakopaji kwa kuwape elimu namna ya kurejesha ili wengine waweze kukopa kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa ziwafikie wote.
Katika kukabiliana na utatuzi wa changamoto za uhaba wa fedha Halmashauri imeingia mkataba na benki ya TID ili iweze kuwa inakopesha wajasiliamali wilayani mpanda ili kuondoa tatizo la ukosefu wa fedha, Mkakati mwingine ni Halmashauri kukikwezesha kiwanda cha uzalishaji mafuta cha Mpadeco, kuweza kusaidia kupatiwa malighafi kwa kutumia mashamba ya alizeti ili kutoa malighafi kwa ajili kuzalisha mafuta kwenye kiwanda hicho na ili waweze kuunza mafuta badala ya alizeti na kuongeza thamani ya mazao.
Naye Afisa maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mpanda Tibenderana Justini alieleza kuwa Halmashauri yake imejitahidi sana kuwawezesha akinamama na vijana kuwapa mikopo zaidi ya shilingi milioni 190 na wafanyakazi wa Idara hiyo wanapata msaada mkubwa kutoka kwenye Halamshauri kuwafikia akinamama vijijini na makundi ya vijana kuwahamasisha kujiunga katika vikundi vya uzalisjai mali.
Mbali ya shughuli hiyo elimu imetolewa kwa wananchi kuhusiana na suala la maendeleo ujenzi wa nyumba bora,usafi wa mazingira, uanzishaji wa vikundi vya uzalishaji mali,vikundi vya ufugaji nyuki ,elimu inatolewa yajuu ya kuelimisha jamii kutokana na ukatlii kwa watoto na unyanyasjai wa wanawake na watoto,utatuzi wa migogoro katika familia kupitia maafisa ustawi wa jamii.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu alikabidhi hundi kwa Halmashauri kwa ajili ya fedha za kuwakopesha akina mama waliojiunga pamoja katika vikundi vya uzalishaji mali,kwa Halmashauri za zamani Halmashauri ya Mpanda na Halmashauri ya Mji kila mmoja walkabidhiwa hudi yenye thamani shilingi million 12.na Halmashauri ya Nsimbo ilikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni Saba kwa ajili ya avikundi vya akina mama na Vijana.
Kwa nyakati tofauti wakurugenzi wa Halmashauri hizo walishukuru kwa msaada huo wa wizara ya Maendeleo kuwapatia fedha hizo zitasaidia kuongezea na fedha za ndani kuweza kuwakopesha wajasilimali akinamama na vijana waweze kuondokana na umasikini kwa kuwawezesha mikopo ili kuanzisha shughuli za uzalishaji mali.
Akiongea kwa niaba ya wakurugenzi wenzao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Rashid Neneka alishukuru Katibu Mkuu kwa kuwawezesha hundi yenye thamani ya shilingi milioni saba kwa na kusema imefika wakati mwafaka na itasaidia kusukuma na kupunguza tatizo la fedha za kuwawezesha kuwajengea uwezo akina mama kwenye vikundi vya uzalishaji mali kwa kuwaondolea umasikini akahidi kuwafedha hizo zitawafikia walengwa kwa wakati kama zilivyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment