Tuesday, February 18, 2014

JIMBO LA KIGAMBONI WAPATA VIONGOZI WAPYA WA CCM

Wajumbe waMkutano mkuu wa CCM wa uchaguzi wa jimbo la kigamboni wakiwa wenye nyuso za furaha siku ulipofanyika uchaguzi huo kwenye ukumbi wa chuo cha Mwalimu Nyerere, Kigamboni.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Ndugu Yahaya Sikunjema akifungua rasmi mkutano wa CCM wa uchaguzi wa jimbo la kigamboni mbele ya Wajumbe wa mkutano huo. Kutoka kushoto kwenye meza kuu ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Ndugu Faustine Ndugulile, Katibu wa wilaya Temeke, Ndugu Robert Kilenge. Picha na Emmanuel J. Shilatu
Mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa jimbo Ndugu Isack Mahela akiomba kura mbele ya wajumbe 60 waliohudhuria mkutano wa uchaguzi wa jimbo la Kigamboni.
Mgombea pekee wa nafasi ya ukatibu wa jimbo la kigamboni Ndugu Abdallah Chachala akiomba kura mbele ya wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa jimbo la kigamboni. Ndugu Chachala alikuwa akitetea tena nafasi yake ya ukatibu wa jimbo la Kigamboni.
Wasimamizi wa uchaguzi huo wakigawa karatasi za kupigia kura kwa wajumbe wa mkutano huo.
Mjumbe wa Mkutano wa uchaguzi wa jimbo la Kigamboni kupitia Chama cha Mapinduzi, Ndugu Emmanuel John akipiga kura yake.
Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa jimbo la Kigamboni wakikusanya kura zao mbele ya msimamizi wa uchaguzi Ndugu Oliver Mwambope
Hatimaye matokeo yalitangawa rasmi ambapo Ndugu Isack Mahela (kushoto) alipata kura 59 za NDIYO huku kura moja ikiharibika, na Ndugu Abdallah Chachala (kulia) alipata zote 60 za NDIYO na hivyo kuwafanya kuwa viongozi wapya wa jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi. Nyuma yao ni Katibu Mwenezi wa CCM (W) Temeke Ndugu Masunu.
Katibu mteule wa Jimbo la Kigamboni Ndugu Abdallah Chachala akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani) kwa kumchagua na kuufanikisha salama mkutano huo wa uchaguzi.
Mwenyekiti mpya wa jimbo la Kigamboni Ndugu Isack Mahela naye pia aliwashukuru wajumbe na kisha kuufunga rasmi mkutano wa uchaguzi wa jimbo la Kigamboni. Wengineo wanaoonekana pichani ni viongozi wa Wilaya ambapo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM (W) Temeke, Ndugu Yahaya Sikunjema, Katibu Mwenezi wa CCM, Ndugu Masunu na Mjumbe wa Kamati ya siasa (W) Temeke, Ndugu Oliver Mwambope. Picha zote na habari Emmanuel J. Shilatu.

No comments: