Wednesday, February 12, 2014

JESHI LA MAGEREZA LAZINDUA DUKA LENYE BIDHAA ZA BEI NAFUU MBEYA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la bidhaa zenye gharama nafuu (Magereza Duty Free Shop) katika Gereza la Ruanda Mkoa wa Mbeya.

Kamishina wa Magereza Nchini, John Minja, amesema Jeshi la magereza limejipanga kuhakikisha linasambaza maduka kama hayo nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa maafisa na Askari ambapo hadi sasa Jeshi hilo limefikisha maduka Sita

Mkuu wa magereza mkoa wa Mbeya  SACP _ J.M. Sang'udi akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa

 Mkurugenzi Mtendaji wa Transit Military Shops(Mtoa huduma ya vyombo vya ulinzi kwa Majeshi ya Tanzania), Alfazar Meghji akitoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kendelea kumpa mikataba ya kufanya kazi Tanzania.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwazkil pamoja ns Kamishina wa Magereza Nchini John Minja wakifunua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa Duka la Magereza 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwazkil akikata utepe kuzindua Duka la magereza (MAGEREZA DUTY FREE SHOP)

MAGEREZA DUTY FREE SHOP


Mkuu wa magereza mkoa wa Mbeya  SACP _ J.M. Sang'udi akiteta jambo na Kamishina wake John Minja


Maafisa mbalimbali wa Magereza walikuwepo katika uzinduzi huo

Wageni waalikwa toka Taasisi mbalimbali walikuwepo katika uzinduzi huo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwazkil akitembelea duka hilo mara tu baada ya kulizindua 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Transit Military Shops akimfafanulia jambo katibu Mkuu wakati wa kutembelea Duka hilo





Mkuu wa polisi mkoa wa Mbeya  Ahmed Msangi pamoja na viongozi wengine wakifurahia kuzinduliwa kwa Duka hilo

Baadhi ya familia za Askari magereza na polisi wakisubiria kuingia ndani ya Duka hilo



Baadhi ya maafisa wa Magereza wakipata maelezo mafupi toka kwa moja ya wasimamizi wa Duka hilo




Picha ya pamoja

Na Mbeya yetu
ASKARI wa vyombo vya Ulinzi na nchini wametakiwa kutumia fursa ya maduka yenye bidhaa zenye gharama nafuu(Duty Free shop)zilizofunguliwa katika Magereza mbali mbali ili kupata vifaa vya ujenzi katika kujenga makazi yaliyobora nay a kudumu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwazkil, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka la bidhaa zenye gharama nafuu (Magereza Duty Free Shop) katika Gereza la Ruanda Mkoa wa Mbeya.
Amesema mpango wa kufungua na kuanzisha maduka hayo ni azma ya serikali ya kuruhusu mpango huu kwa watumishi wanaohudumia katika sekta ya ulinzi na usalama kuwasaidia kuepukana na kadhia waliokuwa wakiipata awali.
Amesema maafisa na watumishi wakitumia vizuri fursa ya maduka hayo katika bidhaa za vifaa vya ujenzi itasaidia kuepuka aibu inayoweza kuwapata maaskari wengi baada ya kustaafu kazi kutokana na kukosa nyumba bora ya kuishi.
Ameongeza kuwa Maafisa na Askari wanaostahili kupata huduma katika maduka hayo wanatakiwa kuzingatia masharti, kanuni na taratibu mbali mbali zilizopo na zitakazotolewa mara kwa mara kuhusiana na utoaji wa huduma husika ili ziweze kuleta mabadiliko makubwa sasa(Big Result Now) kutokana na kuwa na bei nafuu kuliko maduka mengine.
Kamishina wa Magereza Nchini, John Minja, amesema Jeshi la magereza limejipanga kuhakikisha linasambaza maduka kama hayo nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa maafisa na Askari ambapo hadi sasa Jeshi hilo limefikisha maduka Sita.
Ameyataja maduka hayo kuwa ni pamoja na Gereza la Ruanda lililofunguliwa jana Mkoani Mbeya, Ukonga-Dar Es Salaam,Isanga- Dodoma,Karanga- Kilimanjaro, Chuo KPF-Morogoro na Butimba- Mwanza.
Minja amesema kwa mujibu wa sheria ya uendeshaji wa maduka hayo, wanaostahili kupata huduma ni watumishi wa Jeshi la magereza pamoja na familia zao ambapo utaratibu utakaotumika kupata huduma hizo ni vitambulisho vyao vya kazi ili kuhakikisha kanuni na utaratibu wa uendeshaji wa maduka unazingatiwa ipasavyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Transit Military Shops(Mtoa huduma ya vyombo vya ulinzi kwa Majeshi ya Tanzania), Alfazar Meghji ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kendelea kumpa mikataba ya kufanya kazi Tanzsania.
Amesema Military Transit Shop itaendelea kushirikiana na uongozi wa Jeshi la Magereza katika kusambaza huduma ya Duty Free Shop katika Magereza yote Tanzania bara ili kuhakikisha kuwa maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wanaweza kupata manufaa mazuri na bora.
Hata hivyo akitoa shukrani kwa niaba ya Wageni waalikwa katika Sherehe za uzinduzi wa duka hilo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Jaji Samweli Chocha amepongeza jitihada za jeshi hilo katika kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na maisha mazuri.
Ameongeza kuwa pamoja na vigezo na masharti yaliyowekwa katika upatikanaji wa Huduma ni vema Jeshi hilo likaangalia upya umuhimu wa wakazi wanalizunguka eneo hilo namna ya kufaidika na bidhaa zilizomo Dukani kutokana na kutamanishwa na ubora wake.



No comments: