Mama
wa Mitindo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa
onyesho la Lady in Red, Bi. Asia Idarous Khamsin akizungumza na wadau
tasnia ya mitindo waliojumuika kwenye After Party ya kuwashukuru wadau
waliotoa michango mbalimbali tangu kuanza kwa onyesho la Lady in Red
nchini Tanzania.
Na Andrew Chale
HALFA
maalumu ya kilele cha Miaka 10 ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red
Super Brand’ usiku wa Jumamosi Februari 22, lilikuwa la aina yake kwa
kuvutia watu mbali mbali ndani ya Ukumbi na mgahawa wa kisasa wa
Nyumbani Lounge, ambapo pia wadau walikabidhiwa vyeti.
Tukio
hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa wakiwemo wadau wa
ubunifu na mitindo nchini pamoja na watu maalufu, Pia walipata kupita
kwenye zuria jekundu (red carpet) na kupata picha za ukumbusho wa tukio
hilo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho hilo
kila mwaka, Asia Idarous Khamsin, aliwashukuru wadau waliojitokeza
kwenye halfa hiyo maalumu na kutoa vyeti kwa watu na taasisi zilizoweza
kuliunga mkono onyesho hilo pamoja.
Mama
wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin akipozi wakati wa zoezi la kugawa
vyeti na models waliovaa mavazi yaliyoonyeshwa kwenye onyesho la
kutimiza miaka 10 la Lady in Red lililofanyika hivi karibuni.
“Tunamshukuru Mungu kwa kufikisha Miaka 10 ya Lady in red, hadi
kufikia hapa, tumeweza kufanya mambo makubwa katika tasnia hii ya
ubunifu wa mavazi na jukwaa hili litaendelea kuwa chachu ya mafanikio
zaidi na zaidi” alisema Asia Idarous.
Na
kuongeza kuwa, jukwaa hilo ndilo pekee lililoweza kuibua wabunifu
wakubwa hapa nchini huku wengine wakipeperusha vyema bendera ya
Tanzania nje ya nchi, wabunifu hao ni pamoja na Ally Rehmtullah, Martin
Kadinda, Ahmed Abdul, Faustin Simon.
Mwanamitindo
wa siku nyingi Fiderine Iranga akipokea cheti kutoka kwa Mama wa
mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya
mitindo nchini.
Wengine ambao nao wanachipukia kwa sasa akiwemo Salim Ally, Salim Ally, Abdul Mwene,Baby Julieth, Baby Masai na wengine wengi.
Asia
Idarous alibainisha kuwa, wapo mbioni kuliboresha jukwaa hilo na kuwa
la Kimataifa ikiwemo kushirikisha wabunifu wa kimataifa na kufungua
milango kwa wabunifu wa ndani kujiuza kimataifa.
Mwanamitindo
mkongwe Fiderine Iranga akimkabidhi zawadi Mama wa Mitindo Bi. Asia
Idarous kwenye After party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe
za kutumiza miaka 10 ya onyesho la Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa
juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar.
Aidha,
katika halfa hiyo pia wageni na wadau waliofika walipata kushuhudia
shoo fupi ya mavazi yaliyobuniwa na Lucy Warere wa Tifu tifu fashions,
Beda Masai na Asia Idarous Khamsini.
Asia
Idarous aliwataja wadhamini waliodhamini halfa hiyo ni pamoja na Times
fm, Michuzi media group, MOblog, DTV, Nyumbani Lounge, Darling air, G
one Media, Channel Ten, CTN na wengine wengi.
Mbunifu
wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah akipokea cheti cha shukrani ya
ushiriki wa onesho la Lady in Red kutoka kwa Mama yake Mlezi Asia
Idarous Khamsin.
Cake
ya After Party ya Onesho la Lady in Red iliyoandaliwa maalum kwa
kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha sherehe za miaka 10 ya Lady
in Red nchini.
Honest
Arroy wa 360 Degrees akikata cake kwa niaba ya wadau kwenye After Party
ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani
Lounge.
Model
Richard akililishwa kipande cha cake na Mama wa Mitindo Asia Idarous
Khamsin kama shukrani ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya Lady in Red.
Wadau
mbalimbali waliojitokeza kwenye After Party ya kusheherekea miaka 10 ya
Lady in Red wakitazama matukio mbalimbali kwenye luninga ndani ya
kiota cha Nyumbani Lounge.
Mwandishi
wa gazeti la Tanzania Daima, Andrew Chale akilishwa kipande cha cake na
mmoja wa Models kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha
tangu kuanzishwa onesho la Lady in Red mpaka leo hii kutimiza miaka 10
kwenye tasnia ya mitindo nchini.
Wadau
wakiwa wamepozi kwenye kiota cha Nyumbani Lounge wakati wa After Party
ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mdau akipata Ukodak na Models.
Mama
wa Mitindo nchini Asia Idarous Khamsin akipata ukodak na mwanamitindo
Mustafa Hassanali kwenye After Party ya kuwashukuru wadau walioshiriki
kwenye onesho la Lady in Red lililotimiza miaka 10 hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment