Timu zote mbili zikisalimiana
Salaam
Picha ya pamoja ya Waaamuzi wa Kagera Sugar na Mbeya City
Timu Kapteni na waamuzi wakiteta kabla ya mtanange
Picha ya pamoja
Kikosi kilichoanza cha Mbeya City Kikosi cha Mbeya City kikiomba leo katikati ya uwanja muda mfupi kabla ya mtanange kuanza
Taswira kabla ya mtanange kuanza
Mashabiki wa Mbeya City wakiutazama mpira leo Kaitaba mapema kipindi cha kwanza
Hapa ni ushindi tuu ...tunataka .....hatukuja kutafuta sare!!! ilisikika nyimbo kutoka kwa mashabiki!!!
Kutokana na Marekebisho ya Uwanja wa Kaitaba, wadau wakiwa safi kwenye siti zao kuangalia mtanange wa Kagera Sugar na Mbeya City
Kipa wa Kagera Hannington ameumia mguu na amelazimika kutoka nje ya uwaja na nafasi yake kuchukuliwa na kipa Adam Oseja
Ilimchukua muda na baadae watoa Huduma walimtoa baada ya kuona hajiwezi katika kutembea na kwenda kumpa huduma ya kwanza nje ya uwanja.
Mbeya City wakifanya mabadiliko
Patashika kuutafuta mpira
Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao lao lililofungwa na Richard Peter katika dakika ya 72 kipindi cha pili.
Richard Peter akipongezwa na mwenzake baada ya kufunga bao na kuiwezesha Mbeya City kuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Hapa kipa wa Mbeya City nae aliumia lakini aliweza kuamka na kuendelea na kabumbu kama kawa!!Mashabiki wa Mbeya City wakiuzunika baada ya kipa wao kuumia!
Huku Majanga!!! huko vipi!!!Kocha wa Mbeya City Juma Mwambosi akiongea na mwandishi wa TBC1 kwenye uwanja wa Kaitaba baada ya mpira kumalizika Kagera Sugar wakiwa hoi kwa kichapo cha bao 1-0.
Baada ya mtanange kumalizika wachezaji wote wa Mbeya City wakifanya mazoezi kama vile mtanange ndio unaanza !!
Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Mbeya City leo imeanza msimu wa pili vyema baada ya kuifungia Kagera Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani kaitaba bao 1-0. Kipindi cha kwanza kilimalizika kikiwa hakuna timu iliyokuwa imeziona nyavu za mwenzake hivyo zikalazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0, Huku kipa wa Kagera Sugar Hannington akiwa hoi kwa kuumia mguu baada ya kuachia frii kiki na kushtuka mguu na kulazimika kutolewa nje katika kipindi hicho cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 72 Mbeya City wamepata bao kupitia mchezaji wao Richard Peter aliyekuwa amevaa jezi no. 13 mgongoni.
No comments:
Post a Comment