Friday, January 17, 2014

RAIS WA TFF AKITEUA KITUO CHA ALLIANCE ACADEMY KUWA KITOVU CHA MAANDALIZI YA U17 WA MWAKA 2019

ZIARA ya Rais wa TFF Jamal malinzi hatimaye imemelizika leo hapa jijini Mwanza kwa matukio mawili makubwa kufanyika.

Tukio la Kwanza limefanyika majira ya saa 2:30 katika ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza ambapo Shirikisho hilo limesaini mkataba kati yake na Halmashauri hiyo kwaajili ya kuboresha uwanja wa Nyamagana.

Ili ipate kumwaga fedha zake za msaada kiasi cha dola laki 5 ambapo nyingine dola laki 1 zitatoka Halmashauri ya jiji la Mwanza, FIFA  ilikuwa ikitaka uthibitisho toka TFF kuwa uwanja huo kwa miaka yote utatumika kwa matumizi ya michezo yaani soka na si vinginevyo  kwaajili ya kuanza uboreshaji wa uwanja huo uliokuwa na utata wa kutaka kubadilishwa matumizi.

Tukio la pili Malinzi na timu yake ya wataalamu toka TFF, majira ya saa 4 asubuhi imetembelea na kukikagua kituo cha elimu na soka cha Alliance Academy ikiwa ni mwanzo wa mpango wa kitaifa wa kuwekeza katika soka la vijana. BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA KAMILI.
 
Rais wa TFF Jamal Malinzi (katikati mwenye miwani) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa kituo cha Elimu na Ukuzaji vipaji vya michezo cha Alliance Academy James Bwire (kulia) akikagua mabweni ya wavulana ya kituo.
Rais wa TFF Jamal Malinzi (wa pili kutoka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora (wa kwanza kushoto), mkurugenzi wa kituo hicho James Bwire (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa kitengo cha michezo (kushoto) wakifurahia jambo ndani ya moja kati ya mabweni ya wavulana Alliance Academy.
Msafara wa rais huyo pia uliambatana na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Vijana wetu hulala hapa.
Bweni vyumba baada ya vyumba.
Tofauti na eneo la kukaa watazamaji kwa kila kiwanja, katika eneo hili vimeunganika viwanja viwili vyenye ukubwa wa mita 100 kila kimoja (nazungumzia maeneo ya kuchezea) na kingine kilichopo eneo la mabweni ya wasichana, ambapo TFF kupitia rais wake Jamal Malinzi imeahidi kuvikarabati viwanja hivi kwa kuvisawazisha kwa greda, kuviwekea magoli ya kisasa, kuweka udongo wenye rutuba na kuviwekea nyasi za kupanda zenye kiwango.
Shule ya Alliance Academy imeongeza eneo hili lenye ukubwa wa hekta takribani 600 ambapo kunajengwa vyumba vya madarasa, ukumbi wa mikutano na ofisi kwa walimu.
Ujenzi ukiendelea ukumbi wa mikutano.
Majadiliano.
Hili ni eneo jingine na majengo haya ni mabweni ya wasichana Shule ya Secondary Alliance Academy Mwanza.
Msafara umefika hapa katika kiwanja cha soka wasichana ambapo ni moja kati ya viwanja vitakavyo kutana na mpango wa maboresho wa TFF utakao anza haraka wiki chache zijazo.
Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) hapa alikutana na Mwakilishi wa vilabu mkoa wa Mwanza ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Kariuwa ya mkoani Tabora, John Kadutu (kushoto) ambapo walikumbushana mambo mawili matatu na kufurahi kwa pamoja.
Jamal Malinzi alipata fursa ya kuzungumza na wachezaji na wanafunzi vijana wanaochukua masomo ya usimamizi na uamuzi wa michezo (marefa), kikubwa sanjari na kuzingatia michezo pia alisisitiza kuiweka elimu mbele. 
Jiografia kuelekea ofisi kuu za kituo.
Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima akisoma risala mbele ya rais wa TFF Jamal Malinzi na wajumbe wake walio hudhuria ziara ya rais huyo shuleni hapo.
Moja kati ya Madhumuni ya kuanzishwa kwa kituo hiki ni pamoja na:-
1. Kujenga, kuimarisha, kuelimisha na kukuza vipaji vya vijana wa kike na wakiume katika michezo mbalimbali na kukuza michezo hiyo kwa manufaa yao na watanzania kwa ujumla.

2. Kuanzisha, kuendesha na kuendeleza vituo vya michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na semina na makongamano kwa vijana hapa nchini Tanzania.

3. Kuandaa mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

4. Kuwajengea vijana uwezo wa kujiamini kwa kuwapa maandalizi bora kimichezo na kitaaluma katika kufikia lengo lililokusudiwa.

LENGO KUU / MAHUSUSI
Kuhakikisha kuwa kituo kinakuwa bora na mfano wa kuigwa Afrika.
Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima akimkabidhi risala rais wa TFF Jamal Malinzi mbele ya wadau waliohudhuria ziara ya rais huyo shuleni hapo.
Rais wa TFF Jamal Malinzi akimkabidhi mpira Captain wa Mwanza Starehe Club ambaye pia ni mwenyekiti wa uwanja wa CCM Kirumba John Tegete.
Pia Rais wa TFF Jamal Malinzi alikabidhi mipira 10 kwa Katibu mkuu wa Alliance School Sports Academy (ASSA) Bi. Mariam D. Lima kwaajili ya matumizi ya kituo.
Picha ya pamoja.

1 comment:

Anonymous said...

KITUO HIKI KINAMILIKIWA NA NANI?