Faustine Ruta, Bukoba
Alhamisi ya leo Daraja la Mto Kanoni linalounganisha Manispaa ya Bukoba na Wilaya nyingine na pia likitumika kama njia kuu ya kwenda Nchi jirani limezinduliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIAN MASSAWE.
Daraja hili lilikuwa kwenye ukarabati takriabni miezi nane sasa ambapo watumiaji wa vyombo vya moto walikuwa wakilazimika kupitia kwenye Barabara ya muda ya Nyakanyasi, Migera au Kashura kuingia katika Manispaa ya Bukoba.
Limekamilika sasa. Pongezi kwa Tanroads Kagera na karibu Bukoba.
Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE amezindua Daraja la Kanoni hii leo Asubuhi. Na hapa alikuwa akijiandaa tayari kwa kukata utepe
Safi....Tayari Uzinduzi
Mkuu wa mkoa wa KAGERA (kulia), Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE amezindua Daraja la Kanoni hii leo Asubuhi.
Viongozi mbalimbali wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika leo asubuhi saa 2:00
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE (kushoto) akiwa sambamba na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani leo kwenye uzinduzi wa Daraja la Mto kanoni
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe akiteta na Wananchi wa Bukoba kuhusu Uzinduzi huo akisisitiza swala zima la usafi kwa ujumla.
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe akiwapungia na kuwasalimia wananchi wa Bukoba waliohudhulia uzinduzi huo wa daraja la kanoni hii leo
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE leo kwenye uzinduzi wa Daraja.
Daraja hili lilikuwa kwenye ukarabati takriabni miezi nane sasa ambapo watumiaji wa vyombo vya moto walikuwa wakilazimika kupitia kwenye Barabara ya muda ya Nyakanyasi, Migera au Kashura kuingia katika Manispaa ya Bukoba.Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani nae alikuwepo kwenye uzinduzi huo
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe na Viongozi wengine wakipita juu ya daraja hilo la Kanoni lililozinduliwa hii leo Asubuhi.
Mkuu wa mkoa wa KAGERA Kanali mstaafu Fabian Massawe (katikati) kulia ni Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani wakipita juu ya Daraja kwa furaha leo kwenye uzinduzi wa Daraja la Mto kanoni
Pongezi kwa Tanroads Kagera na karibu Bukoba.
No comments:
Post a Comment