Friday, January 24, 2014

MAMA KANUMBA AKUTANA NA KUNDI LA WASANII WA BUKOBA LEO


Na Faustine Ruta, Bukoba
Mama Flora Mtegoa, mzazi wa  muigizaji Marehemu Steven Kanumba,  akionekana mwingi wa furaha leo baada ya kukutana uso kwa uso na wasanii wa nyumbani Bukoba leo kwenye Fukwe za Kiroyera ziwa Victoria. Wasanii hao pamoja na kukutana na Mama Kanumba walikuwa kwenye matayarisho ya Uzinduzi wa Filamu yao mpya.
Mama Kanumba (kulia) akisikiliza swali kutoka kwa Msanii
Msanii akimuuliza swali Mama Kanumba
Dada Jesca na Onyango
Mama Kanumba.
Mama Kanumba akifunguka na kuwaelezea mambo mbalimbali kuhusu tasnia hiyo pendwa hapa Tanzania
Wasanii kwa pamoja wakiongea leo na Mama Kanumba ambeye yupo hapa Kagera kwa siku ya tatu sasa.
Msanii wa Maigizo  Jesca akimsikiliza kwa makini Mama Kanumba leo kwenye Fukwe za Kiroyera katika Ziwa Victoria.
Teso Boy kulia nae alikuwepo sehemu hiyo ya Kiroyera Beach kumsikiliza Mama yake na Kanumba ambapo wameongea mambo mengi. 


kushoto ni Teso Boy na katikati ni Madoo

1 comment:

Anonymous said...

Kitu kinachonifurahisha kuhusu sisi watz ni ukiangalia huo mjumuiko hapo inaonekana kama wa kikazi vile, LAKINI naona kuna watu wanakata kilaji, sasa huyo mheshimiwa anayemuuliza swali huyo mgeni rasmi atakuwa ana uhakika gani kama amejibiwa kisahihi (correctly)? Maana unavyokuwa umeweka angalau hata glasi moja ya kilevi lazima itaathiri ubongo angalau kwa kiasi fulani (utakuwa hyper au hypo). Kwa uelewa wangu na kufanya kazi nchi mbalimbali sijaona wakati wa kazi au majadiliano yoyote yale yanasindikizwa na pombe hata kama linalojadiliwa ni social issues, nachojua baada ya mkutano watu wanajumuika pamoja na hapo hakuna maswali au majibu kunakuwa ni kusherekea tu. Sijui labda nchini kwetu ni tofauti.