Wednesday, January 8, 2014

DKT. SHEIN KATIKA UZINDUZI WA TAASISI YA MWAHARAKATI BIBI SITI BINTI SAAD

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,alipohudhuria katika Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel jana,ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya mapinduzi Ya zanzibar (katikati) Bibi Nasra Mohamed Halal Mwenyekiti wa Taasisi.
Watoto wakiimba nyimbo mbali mbali za michezo ya kizamani ikiwemo nyimbo ya ukuti,wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi ni miongoni mwa Wananchi waliohuduria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,taasisi hiyo iliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wananchi waliohuduria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wananchi kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja walihuduria katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel (pichani) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akihutubia jana, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(kushoto) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad akifuatiwa na Mwenyekiti wake Bibi Nasra Mohamed Halal, wengine kulia Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk,wakiwa katika Uzinduzi wa Taasisi hiyo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hote, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Prof Laura Fair, aliyefanya utafiti na kutunga kitabu cha wa mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akizindua kitabu hicho wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya mwanaharakati huyo iliofanya jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shei,(hayupopichani) katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel mjini Unguja,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Historia ya Harakati za wanawake iliyotolewa na Dk.Amina Ameir,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na kumpongeza Dk.Amina Ameir,baada ya kutoa Historia ya Harakati za wanawake katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Viongozi wengine wakiangalia picha ya Bibi Siti Binti Saad,iliyokuwa ikipigwa mnada katika uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saa,Bibi Nasra Mohamed Hilal,alipomkaribisha mlezi wa taasisi hiyo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,kuzungumza machache ili nae amkaribishe mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kutoa hutuba yake na kuizindua rasmi katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimshukuru Muharami Mohamed,Kitukuu cha Bibi Siti Bnti Saad,baada ya kumpa zawadi ya kofia aliyoivaa,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,(akiyesimama) akiwa mlezi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad,akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kuizindua taasisi hiyo katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Viongozi na wananchi wakati alipozindua Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisoma maandishi yanayosomeka "TAASISI YA MWANAHARAKATI BIBI: SITI BINTI SAAD"mara baada ya kufanya izinduzi wa Taasisi hiyo jana katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimakabidhi Picha ya Bibi Siti Binti Saad,Nasib Amour,kwa niaba ya Zanlink,ambayo ilyonadishwa na kufikia bei ya Tsh Laki Tano,pia zanlink itawaunganishia Mtandao wa Internet kwa mwaka mmoja,wenye gharama ya Dola Elfu moja na Nusu,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimakabidhi Picha ya Bibi Siti Binti Saad,Mbunge wa Jimbo la Mpendae Salum Turky,aliyoinunua kwa mnada kwa bei ya Tsh Millioni Moja, wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimakabidhi Picha ya Bibi Siti Binti Saad,Prof Martin Mhando,mwanakamati katika taasisi, iliyonadihswa kwa bei ya Tsh laki mbili na Hamsini Elfu,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Binti Saad katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Kikundi cha Taarab asilia cha Rahatu zamani,kikitoa burudani yao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad,katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,(pichani) Muharami Mohamed,kitukuu akiimba moja ya nyimbo za Marehemu Bibi Siti Binti Saad.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja iliyowajumuisha Viongozi wakuu wa Serikali na wasanii wa Kikundi cha Taarab asilia cha Rahatu zamani,wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad,katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa katika picha ya pamoja iliyowajumuisha Viongozi wakuu wa Serikali na wana kamati wa uzinduzi wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti Bnti Saad,katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Hotel Mjini Unguja jana,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments: