Friday, January 10, 2014

ASKARI POLISI NA ASKARI MAGEREZA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA MBEYA

Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
Mwenye Jaketi la Njano ndiye Mshitakiwa namba moja PC James.
Ulinzi ukiimarishwa Baada ya watuhumiwa wa ujambazi kufikishwa mahakamani
Mbele ni mshitakiwa wa nne Mbaruku Hamis akiingia mahakamani
Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshitakiwa wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini , Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .
Wa kwanza kushoto aliye vaa shati la Draft ni Dereva Ezekia Matatila (34) pamoja na wasikilizaji
Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha 
Katikati ni Mke wa mshitakiwa wa tatu ambaye ni Askari Magereza Sajini Juma Mussa, Hata hivyo mwanamke huyo alizirai mahakamani wakati mumewe akiwa kizimbani.

ASKARI wawili wa jeshi la Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni raia wa kawaida wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya wakituhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.

Watuhumiwa hao watano kwa pamoja walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite wakituhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya kuhukumiwa kijeshi.

Aliwataja wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.

Akisoma mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, Mulisa alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.

Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 AINA YA Grand Mark II.

Aliongeza kuwa mbinu iliyotumika ni watuhumiwa ni watuhumiwa hao kutega magogo barabarani huku wakiomba msaada kwa madai kuwa magari yao yameharibika na ndipo baada ya wahanga kusimama waliwapora vitu vyao wakiwa na mapanga ambavyo ni pesa shilingi Milioni 3.5, Mabegi matatu yenye nguo mbali mbali yenye nguo, Kompyuta mpakato, simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Shilingi Laki mbili pamoja na simu ya Dereva aina ya Tekno ambayo aliitambua Mahakani na kutumika kama kielelezo.

Hata hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na matukio hayo ambapo upande wa Mashtaka ulileta Shahidi mmoja ambaye ni Dereva wa Pick up Ezekia Matatira ambaye aliwatambua washtakiwa wote watano na kuiambia mahakama kuwa siku hiyo ya Tukio aliagizwa na Bosi wake kwamba awapeleke wageni Chunya na ndipo alipotekwa katika eneo hilo huku watekaji wakiagizwa na Maaskari na yeye kufungwa  pingu na kutishiwa na panga.

Aidha kutokana na kesi hiyo Hakimu Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 15, mwaka huu ambapo upande wa Mashtaka utaleta mashahidi wengine huku watuhumiwa wakirudishwa Rumande baada ya dhamana yao kufungwa.

Ezekiel Kamanga

Mbeya yetu Blog

No comments: