Monday, December 9, 2013

WADAU ERICK 'MSENGII' NATIANOTA NA HERIETH WAMEREMETA

Bwana Harusi Erick 'Msengii’ Natianota akimlisha keki mke wake kipenzi Herieth Kashangaki wakati wa tafrija ya kumeremeta kwao siku waliyoamua kuachana na ukapela mwishoni mwa wiki.
Baba mzazi wa Bwana harusi Mzee Shanta Natianota,akiongea machache kwa wanae Erick na Herieth.
Wafanyakazi wenza na Bw.Harusi wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wageni waalikwa..
Mrs Nkurlu akitoa hongera kwa waliomeremeta.
Hongera mdogo wangu alisikika akisema Bro Joe.
Mambo ya kwaito hayo…saaafi
Wadogo zake bwana harusi wakiwa na nyuso za furaha kwa kaka yao kuoa.
Mama mzazi wa Bw.Harusi akimkabidhi zawadi ya vyombo Bi.Harusi Herieth ili aendelee kumpikia Erick ipasavyo kama yeye alivyokuwa akimpikia mwanae”Mambo ya Siha njema hayo”
Edna Kashangaki ambaye ni dada yake mkubwa na bi.Harusi akilia kwa furaha mara baada ya kuagana na mdogo wake.

No comments: