Kaimu mkurugenzi mkuu wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe ( kulia) akimakabidhi Bi Jane Mwakinyuke kutoka Hifadhi ya Taifa Mikumi , cheti cha kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja ya kuongoza watalii katika hifadhi za Taif
Askari pekee wa kike kutoka hifadhi ya Taifa ya Ruaha Jane Griffin Mwakinyuke ambae amehitimu mafunzo ya kuongoza watalii katika utalii wa miguu hifadhini akionyesha cheti chake |
a ambao hupenda utalii wa miguu juzi ambapo jumla ya askari 20 kutoka hifadhi mbali mbali walihitimu mafunzo hayo,kulia kwake ni Bw Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST'
Na FRANCIS GODWIN BLOG
TANZANIA yazidi kung'ara katika sekta ya utalii barani Afrika baada ya kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kwa kwa kuvutia zaidi watalii katika safari za utalii katika hifadhi hiyo huku hifadhi ya Serengeti na Ruaha Iringa zikiongoza kwa ubora ya utalii.
Kaim mkurugenzi mkuu wa hifadhi za Taifa (TANAPA ) Dr Ezekiel Dembe aliyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja ya kwa askari 20 ,mafunzo ya utalii wa miguu katika hifadhi hiyo ya Ruaha na nyingine kama Mikumi na Udzungwa yaliyofanyika katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa .
Dr Dembe alisema kuwa Tanzania imeonekana ni nchi ya kwanza kwa utalii baada ya wataalum wa masuala ya utalii barani Afrika kuchagua nchi nane barani Afrika ambazo zinafaa kwa kufanya safari za utalii
Alizitaja nchi zilizoshindanishwa kwa kupigiwa kura kuwa ni Tanzania , Botswana , Uganda , Namibia ,Afrika ya kusini , Kenya , Zambia na Zimbabwe na huku Tanzania ikionekana ni nchi inayoongoza kwa safari za kitalii ukilinganisha na nchi nyingine zilizowekwa katika orodha hiyo.
Pia alisema mbali ya kuchagua nchi inayofaa kwa utalii pia wataalam hao walitazama maeneo 50 yaliyofaa kwa safari za utalii na Tanzania ikifanikiwa kupata maeneo 10 bora zikiwemo hifadhi 8 ambazo zipo katika TANAPA na Selous na Ngorongoro huku mlima wa Kilimanjaro haukuwekwa kutokana na hifadhi hiyo ya Kilimanjaro ni maalum kwa kupanda mlima pekee.
Hata hivyo alisema katika hifadhi hizo 10 bora kwa hifadhi za kusini hifadhi ya Ruaha imeongoza ikifuatiwa na katavi wakati hifadhi ya kwanza kwa hifadhi bora ilikuwa ni Serengeti wakati hifadhi ya pili ilikuwa ni hifadhi ya Ruaha barani Afrika ambazo zilionekana ni bora na vinavutia zaidi kwa safari za kitalii.
Dr Dembe alisema kuwa hivi sasa TANAPA wameelekeza nguvu zote katika kuendelea kuitangaza hifadhi ya Ruaha Iringa ikiwa ni pamoja na kubadilisha mazingira ya hifadhi hiyo ili kuvutia idadi kubwa ya watalii katika hifadhi hiyo ambayo ndio hifadhi kubwa kuliko zote katika Tanzania.
Hata hivyo alisema kuwa katika kuboresha utalii wa kusini TANAPA ipo katika mkakati wa kutoa elimu kwa madereva wanaopeleka wageni katika hifadhi mbali mbali ikiwemo hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ili kuona kampuni za kitalii kuwa na madereva ambao wanajua vema utalii na kuepuka udereva wa vurugu katika hifadhi.
Alisema kuwa utalii ni sekta nyeti katika Taifa hivyo lazima wale wote wanaohusika na masuala ya utalii kuwa na elimu ya kutosha juu ya utalii na kuyataka makampuni kuepuka kuwatumia madereva wa daladala kupeleka wageni hifadhini ambao baadhi yao wamekuwa hawana elimu ya utalii .
Kuhusu askari hao 20 waliopewa mafunzo Dr Dembe aliwataka kuwa wazelendo na hifadhi pamoja na Taifa zima la Tanzania na kuepuka kugeuka kuwa maadui wa hifadhi kwa kushirikiana na majangili kuhujumu hifadhi hizo .
Wakati huo huo Dr Gembe alivitaka vyombo vya habari na wanahabari nchini kuendelea kutangaza utalii ikiwa ni pamoja na kuepuka kuandika habari ambazo hazisaidii katika ukuzaji wa sekta ya utalii .
Alisema iwapo vyombo vya habari nchini vitafanya vizuri katika kuhamasisha utalii na kuwa na uzalendo na Taifa la Tanzania katika kuepuka kuandika habari za kutisha wageni kufika katika hifadhi ni wazi sekta ya utalii nchini haitakuwa .
Kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ruaha Bw John Nyamhanga mbali ya kuomba TANAPA kusaidia kumaliza kero ya vitendea kazi kwa askari hao bado alisema kuwa mafunzo hayo ya utalii wa miguu kwa askari hao ni mzuri zaidi japo mafunzo hayo yanaweza kukwamisha upande mmoja katika utendaji kazi wa kila siku katika hifadhi hiyo ya Ruaha .
Kwani alisema kuwa askari hao ndio ambao wamekuwa wakitumika katika shughuli nyingine za hifadhi hiyo hivyo iwapo TANAPA haita ongeza idadi ya watumishi wengine kuna uwezekano wa kupunguza idadi ya watumishi wa idara nyingine .
Godwell ole Meing'ataki Mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao wa maeneneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania. ' SPANEST alisema kuwa lengo la SPANEST ni kuendelea kuboresha zaidi hifadhi ya Ruaha ni nyingine ili kuwavutia zaidi watalii wa ndani na nje kufika katika hifadhi hizo .
No comments:
Post a Comment