MWENYEKITI wa CCM Kata ya Kibamba, Ayoub Semvua akimpongeza Mbunge wa Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, baada ya kuzungumza kama mgeni mwalikwa kwenye Kichao cha kawaida cha Hamlashauri Kuu Kata ya Azimio jimboni humo, jana jioni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Esa Uswege.
=================
BASHIR NKOROMO, TEMEKE, Tanzania
Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Kibamba, Dar es Salaam, Ayoub Semvua, amesifu kuwa kasi ya utendaji kazi ya mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu ni kubwa na huenda inastahili kwendana na kasi ya utendaji wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.
"Nilipoitwa na rafiki zangu hawa wa Azimio, sikujua kama na wewe utakuwepo, lakini nikawa nimenuia kuwa hata kama hutakuwepo nitakusifia kwa kazi kubwa unayofanya ya kimaendeleo katika kutekeleza ilani ya CCM katika jimbo hili la Temeke... na sasa kuwa nimekukuta nitakusifu hapa hapa, wewe kasi yako ya utekelezaji wa ilani ya CCM inatisha, na kwa kasi hii unaweza kuwa unastahili kasi ya viongozi wetu Ndugu Kinana, Mzee Mangula na Kijana wao Nape", alisema Semvua alipopewa fursa ya kuzungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Azimio, ambacho alikuwa mgeni mwalikwa.
"Huyu Katibu wetu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula na kijana wao Nape, kasi yao ni kilometa 140 kwa saa. Kama kuna mtu aliyeingia katika uongozi wa CCM kwa lengo tofauti kasi hii lazima itamshinda na bora ajiondoe mwenyewe mapema", Semvua aliongeza.
Semvua alisema, kutokana na utendaji bora na shirikishi wa Mtemvu, jimbo la Temeke limekuwa na sura tofauti kimaendeleo ikilingtanishwa na miaka 20 ikiongozwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa sasa wa TLP, Augustine Mtema ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.
"Mfano mzuri wa maendeleo, niliyoshuhudia ambao kila mtu anauona ni barabara za lami zilivyotanda katika maeneo mbalimbali ndani ya Temeke, tangu nimetoka Kibamba nimeteleza kwa lami moja kwa moja bila kugusa udongo hadi naingia kwenye Ofisi hii ya CCM Azimio", alisema Semvua.
Semvua alisema, kutokana na kasi inayoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na viongozi wengine kama Mtemvu, CCM itashinda urais ba viti vingi vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2014.
Aliwataka wana-CCM kuachana na tabia ya kuwa na nongwa aliyoifananisha na ya kinywaji cha kahawa, ambayo baadhi wamekuwa wakidumu nayo kiasi cha kuchagua wapinzani wakidhani wameikomoa CCM kumbe wamejikomoa wenyewe.
"Pale wilaya ya Kinondoni tumepoteza viti viwili vya ubunge na vingi tu vya udiwani na mitaa, sababu kubwa ni nongwa tu. Wanasema, Wakasema aaa, bora tuupe upinzani tuheshimiane. Sasa ukiwauliza pale Kawe na Ubungo kwamba mliwapa ubunge wapinzani sasa heshima gani mnapata? hawana jibu zaidi ya kuinama chini", alisema Semvua.
Akifungua kikao hicho, Mtemvu aliwataka wana-CCM na wananchi kwa jumla kuwapima viongozi kwa utendaji kazi zao na sio kwa uhodari wa porojo nyingi kwa sababu wananchi wanachohitaji ni maendeleo.
Alisema, katika kipindi chake cha Ubunge, Temeke imeweza kuwa na barabara karibu 15 zenye lami hadi pembezoni mwa mji huo na kwamba zile zisizokuwa na lami zimeboreshwa kwa kiwango kibwa kiasi cha kupitika nyakati zote.
No comments:
Post a Comment