Friday, December 27, 2013

HIVI NDIVYO WATEJA WA VODACOM WALIVYOJIRUSHA KILA KONA YA JIJI LA DAR WAKATI WA SIKUU YA KRISMASI

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la TMK Wanaume "Chege "akionyesha umahiri wake wa kutawala jukwaa wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei kwaajili ya wateja wao wakati huu wa sikukuu ya Krismasi.
Mmoja wa wasichana waliokuwa wakipromoti simu za Huawei akipita jukwaani huku akionyesha moja ya simu za Huawei wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu, katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Msanii wa kundi la Tiptop Connection Madee akiwaburudisha mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach, wakati wa kusherehekea sikukuu ya krismasi na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei ,wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa kampuni hizo.
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Profesa Jay akiwapagawaisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti kwaajili ya wateja wao wakati huu wa msimu wa sikukuu ya krismasi.
Kiongozi wa bendi ya muziki wa kundila la Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuph akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa Tamasha la Cheka Mbombastik lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live mbagala jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi Tamasha hilo liliandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti.
Umati wa watu waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwaajili ya wateja wake na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu ya krismasi.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Joe Makini akionyesha umahiri wake kwa mashabiki wa muziki huo wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti Breweries katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wao wakati wa msimu huu wa sikukuu ya krismasi.
Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la Changamoto Albart Jackson akionesha simu aina ya Huawei Y210D yenye thamani ya Tsh. 160,000 kwa waandishi wa Habari aliyojishindia kwenye bahati nasibu iliyowahusisha waandishi wa habari,wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu,Kulia ni Mtaalamu wa bidhaa na Vifaa vya simu wa Vodacom Bw.Edwin Byampanju na kushoto ni Meneja Masoko na usambazaji wa Huawei Ramadhani Hamad. 

No comments: