Monday, November 4, 2013

RC ISHENGOMA AZIBANA HALMASHAURI IRINGA KUWASILISHA MFUKO WA BIMA YA AFYA KIASI CHA TSH MILIONI 87 ZA TELE KWA TELE

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma akifungua mkutano wa  siku ya  ya  wadau   mfuko wa bima ya afya mkoa  wa Iringa kutoka  kushoto ni kaimu mkurugenzi wa NHIF Khamis Mdee,mwenyekiti wa bodi ya NHIF  balozi Ali Mchumo  na kulia ni kaimu ras Bw Mwasumile na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu
viongozi  mbali mbali na  wadau  wakiwa katika mkutano  huo  leo katika ukumbi wa St Dominic

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma wa tatu kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  mbali mbali mara baada ya kufungua mkutano wa  siku ya  ya  wadau   mfuko wa bima ya afya mkoa  wa Iringa kutoka  kushoto ni kaimu mkurugenzi wa NHIF Khamis Mdee,mwenyekiti wa bodi ya NHIF  balozi Ali Mchumo  na kulia ni kaimu ras Bw Mwasumile na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu
Viongozi  wa  kitaifa na mkoa  wa Iringa  waliokaa  wakiwa katika picha ya pamoja na  wadau  wa mfuko wa bima ya afya mkoa  wa Iringa leo
Wafanyakazi  wa mfuko  wa bima ya afya  Taifa na mkoa wa Iringa  wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni  rasmi na  viongozi wa mfuko  huo na serikali ya  mkoa wa Iringa leo
Na Francis Godwin Blog
.............................................................................................................................................
MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa Dr Christine Ishengoma  amezitaka  Halmashauri  za  wilaya  katika  mkoa  wa Iringa ambazo  hazijawasilisha madai  ya tele kwa tele yenye  jumla  ya shilingi  milioni 87 kwa  ajili  ya mfuko  wa  bima  ya afya  kuwasilisha  mara  moja.

Pamoja na  kuzitaka  halmashauri  hizo  kuwasilisha  fedha hizo  pia mkuu  huyo  wa  mkoa alitangaza  kuwachukulia hatua kali  watoa  huduma katika  vituo vya afya  ambao  wanahujumu mfuko  huo  wa bima  ya afya kwa  kughushi  huduma  za matibabu za  mfuko huo  na  mingine  ya afya.

Mkuu  huyo  wa  mkoa  alitoa agizo  hilo leo  wakati  akifungua  mkutano  wa siku ya  wadau wa  mfuko wa  bima  ya afya mkoa  wa Iringa  ,uliofanyika katika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa .

Alisema  kuwa  zipo changamoto ambazo  serikali  ya  mkoa  wa Iringa  imepata  kuziona ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi  ikiwemo  changamoto ya uchakavu  wa baadhi ya vituo  vya  serikali kama  vile  Zahanati ya  Isele, Ilolompya,Mapogoro ,Kising'a na Mtandika pamoja na  upungufu wa  dawa hasa katika vituo  vya serikali .

Dr Ishengoma  alisema  kuwa  serikali  imejipanga  kufanyia  kazi  changamoto  hizo japo  alisema  hali ya uandikishaji  wanachama  wapya  wa mifuko  hiyo katika  mkoa  bado  si ya kuridhisha  mbali ya  kuwa  mkoa  wa Iringa unaongoza kwa  kuandikisha  wanachama  wengi  katika Tanzania kwa kuwa nafasi ya nne   kutimiza lengo la kuandikisha  kaya 12,244 hadi juni 30 mwaka  huu ambayo ni  sawa na asilimia 9.6 ya malengo  ya kuandikisha kaya 127,561 ifikapo mwaka 2014/15  .

Pia aliwataka   watoa  huduma  kuhakikisha  wanawapa  huduma  wanachama  wa NHIF na CHF  sawa  na wananchi  wengine bila ya ubaguzi wowote  kwa kuwa mojawapo  ya malalamiko yanayotokana na wanachama  wa  mifuko  hiyo ni pamoja na  kubaguliwa  katika huduma kwa  kuonekana  kama  watu  wanaotibiwa  bure  mtazamo ambao  si sahihi  kwa maana  gharama za  matibabu  kwa  wanachama hao tayari  zimelipwa kupitia  mifuko hiyo.

" Nawaagiza  watoa  huduma  wote  kuacha mara  moja  tabia  hiyo isiyozingatia utu ....watakaobainika  kuwasumbua  wagonjwa  ambao  ni  wanachama  wa mifuko hiyo tutawachukulia  hatua kali  zaidi "alisema mkuu  huyo  wa  mkoa

Katika  hatua  nyingine  mkuu  huyo  wa  mkoa  aliwataka  wanachama  wa mifuko  hiyo  ya NHIF na CHF  kuendelea  kutumia kadi zao  halali na kuachana na mpango wa  kuazimishana kadi za matibabu ama  kufanya  biashara  kwa  kutumia kadi hiyo kwa ajili ya kughushi  huduma za matibabu .
Kwa  upande  wake mwenyekiti  wa bodi  ya NHIF balozi Ali Mchumo(pichani juu)  alisema  kuwa   katika  kuhamasisha  wananchi  wengi  zaidi  kuendelea  kujiunga na mifuko  hiyo unaanzishwa  utaratibu  wa kutoa  tuzo ya bima ya afya kwa  wote kwa wilaya  ambazo zitafanya  vema  katika  kuingiza  idadi kubwa  zaidi ya  wanachama.

 Alisema  kuwa lengo la  serikali  ni kuona  watanzania  wote  wanapata  huduma  bora  ya afya  kwa  kujiunga na mifuko  hiyo  hivyo  ili  kutimiza lengo  hilo ni lazima  kila  kiongozi na kila  wilaya  kufanya  uhamasishaji   ili  kila mtanzania  kujiunga na mifuko hiyo.

No comments: