![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfLLl7CnWEZ5OqrVT1MwH7BxZi3e3huYxo_x5xyU6lYYSqAoLjgGBp3GZG3N5fMyCCGRb-0uZlVQ_28O77Rlk3I144UcnAkiFxMdhsXv6MHN1UY2TQXi3AXcq8a9OzADKOXFhXUS0V31YW/s640/PB216506.jpg)
........................................................
Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa Mikoa iliyowezeshwa kuwa na Miundombinu ya huduma ya "Video Conference" ambao unaratibiwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Huduma hii muhimu itasaidia sana katika kurahisisha mawasiliano Serikalini na hivyo kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi.
Katika majaribio ya awali Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetoa mada mbalimbali kupitia mfumo huo kwa Makatibu Tawala pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mikoa ya Rukwa, Mara, Lindi, Ruvuma na Shinyanga.
Miongoni mwa mada hizo zilizowasilishwa zikifuatiwa na majadiliano ni Utekelezaji wa Mfumo wa "OPRAS" katika Utumishi wa Umma, Mwenendo wa utekelezaji wa masuala Anuai za jamii katika Utumishi wa Umma, Usimamizi na uzingatiaji wa Maadili ya Utumishi wa Umma na Mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini.
Zoezi hili la majaribio limefanikiwa japo kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo kukatika kwa mawasiliano yanayounganisha picha na sauti sababu kubwa ikiwa ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kukosa huduma za Mkongo wa Taifa unaoratibiwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayanisi na Teknolojia.
Changamoto nyingine ni baadhi ya picha kuwa na muonekano hafifu, ambayo kwa mujibu wa Mchambuzi wa Mifumo ya Komputa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Emmanuel Mwandiga inasababishwa pia na kasi ya huduma za mtandao kuwa chini pamoja na masafa ya mawasiliano kuwa hafifu.
Changamoto hizo zikifanyiwa kazi na Wizara husika ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ni wazi kuwa mfumo huo utakua njia sahihi zaidi na kisasa inayokwenda na wakati katika kurahisisha na kuboresha mawasiliano Serikali.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMRHe4vw99MhULTZoJfkRPb4SAP4pggK6DOJTvnF4doQbERxSudny1Mr_ZR7zMn0v71Iow8CPu8_OWO0pc7eq2rfigfjUdfvN8z4YXmXeL28Z82GsZMOiZvZctWZ60whmqceQRK3wkAhV9/s640/PB216510.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkUGilYo49tkmbgRFw8Cxgu39QOjUidmgpuLMiPaO7UeLkNrDgran3Ps8nD0kFOBXrJff_fiY0H5RcR5zZ4qBPE5680EZnMYBoDBrjRT-eRE3E2hj6qwq4Fd1RUKCwlOtc9EMMYR5qWsUF/s640/PB216522.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgg51yJNw7FDaIFxX26L_1HpSD8gOYYRQDDdySo_yK8JjVYsZSeNdk3_CkffJl7IkWZp2QyJWovoywf9oMPrZSXFJCT4v1D0BKTAdb2gqgVTqMuXakU-XmGcg7MNJi-KrgW-ajMRva0_8Af/s640/PB216514.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_djqULuwYdrDBhF8m2MPl27ErFZ2-95StPZdViqLdQ9CIqnByLfXgXXDS3phdkt0pLtZHmxjVwBdUvCotWblhw96lpGYRW1m6IT1OYsJnEbLQznmRM3aWIemLH8lu3vtrWPFl-pTFObk0/s640/PB216515.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRE1D9QOxSuu1SqVqRSaar0HtQnIPRltAQhGjkk-jU81WOzCAuer8rHek3XNa7HPwgiMvpIVmm2yVUf1CYRWk84NgDwep4lBJOjc8h4_XB4A_fN0HoDHKvU1dGYL3BFDuHCHvi1vMeKk9k/s640/PB216524.jpg)
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment