Monday, November 18, 2013

KINANA NA UJUMBE WAKE AWASILI MJINI SONGEA LEO

 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ukipita leo katika 'mkeka' wa barabara, ulipokuwa ukitokea wilayani Namtumbo kwenda wilayani Songea mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana yuko katika ziara mkoani Ruvuma, kukagua utelekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua, barabara hiyo ni miongoni mwa barabara kadhaa zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero ya kusafiri kwenye barabara mbovu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya maabara katika shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
 Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wai Ruvuma, kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Mahilo, Songea mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.

 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazee waasisi pamoja na wananchi wa kata ya Matogoro ambapo alitaka wana CCM kuenzi kazi zilizofanywa na waasisi wetu kwa kudumisha mshikamano ,umoja na amani.
 Ofisi ya Kata ya Matogoro  CCM ambayo iliwekwa jiwe la msingi tarehe 20 Desemba 1986 na Mzee Rashid Mfaume Kawawa,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameahidi kutoa bati za kuezeka ofisi  hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchama wa Shina namba 1tawi la Ambachai kata ya Mfaranyaki nyumbani kwa Balozi wa Shina Ndugu Magreth Mchula,Katibu Mkuu alisisitiza viongozi wa ngazi za chama kuwa na mazoea ya kutembelea mabalozi wao kwani ndio msingi wa wanachama.
 
 Wanachama wa Shina namba 1 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,pichani Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amejumuika na wanachama kukaa nao pamoja kwenye mkeka.

 Mzee Mustafa Mohamed Songambele akionyesha furaha yake alipokutana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mfaranyaki Songea,Katibu Mkuu ameanza leo ziara ya kuetembelea wilaya ya Songea mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumlaki alipowasili kwenye eneo maarufu linalojulikana kama Nonga Nonga wilaya ya Songea mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mzee Mustafa Songambele mmoja wa waasisi wa Tanu na mwanasiasa wa muda mrefu.
 Mlezi wa Vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu vijana hao baada ya kufunguliwa kwa Shina lao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya kutoka kikundi cha ngoma cha Mfaranyaki baada ya kuzindua shina la vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishirikiana na wananchi wa Kata hiyo kusafisha eneo kwenye ujenzi wa Zahanati ya kata hiyo. Wanne kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Wazee pekee wawili walisosalia kati ya waliokuwepo kwenye mkutano wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa harakati za TANU, mwaka 1957 katika eneo la Matogolo, Songea mkoani Ruvuma, Hashim Gawaza (92) na Clemence Simon Nyoni (93), wakivishwa vazi la heshima na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipowasili eneo hilo leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa na wanachama wa Shina namba noja, waliokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa Mjumbe wa Shina namba moja, Magreth Mtiula, eneo la Mfaranyaki mjini Songea.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia mama huyu, Mkazi wa mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea, baada ya kumuona kuwa mwenye shangwe kubwa wakati msafara wa Kinana ulipopita karibu na nyumbani kwa mkazi huyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua Shina la Vijana Wajasiriamali wa CCM la Dk. Asha-Rose Migiro, katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia baada ya kuzinduliwa shina hilo.

No comments: