Saturday, November 2, 2013

CCM NA CPC WAPEANA SOMO DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akifungua semina ya siku 2 iliyoshirikisha Chama Cha Mapinduzi na Chama rafiki cha Kikomunisti cha China  (CPC) katika hoteli ya Courtyard mjini Dar es Salaam. Semina hiyo ilikuwa mahususi katika Kuvijengea Vyama Uwezo  na Umuhimu wa Vijana katika vyama.

 Naibu Mkurugenzi wa CPC katika masuala ya Kimataifa Ndugu An Yuejun akitoa salaam za shukran kwa niaba ya wajumbe wenzake kabla ya kuanza kwa semina ya siku mbili iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.

 Profesa Song Li akitoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kiuchumi ikiwa mipango iliyofanywa na CPC tangu kuanza kwake katika kuboresha na kukuza uchumi wa China.
 Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Ndugu Anamringi Macha akibadilishana mawazo na Makamu Mkurugenzi katika masuala ya Kimataifa wa CPC Ndugu An Yuejun mara baada ya kumaliza semina kwa siku ya kwanza.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (Zanzibar) Salama Aboud na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Bara wakifurahia jambo na Naibu Mkurugenzi wa masuala ya kimataifa wa CPC Ndugu An Yuenjun.
 Katibu wa Mkoa wa Vyuo Vikuu CCM Ndugu Christopher Ngubiagai akitoa mada juu umuhimu wa vijana katika CCM na matatizo yanayowakabili vijana wengi wa Tanzania na kusini mwa jangwa la Sahara katika semina ya siku mbii iliyoanza tarehe 31 Oktoba na kuhitimishwa tarehe 1 Novemba katika hotel ya Courtyard jijini Dar es Salaam na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM na CPC kutoka China.

 Suleiman Mwenda kutoka Idara ya Itikadi na Uenezi akielezea namna internet inavyofanya kazi katika kufikisha ujumbe hasa kwa vijana na pia hatua ambazo serikali inazichukua katika kuboresha na kuzuia upotoshaji ama matumizi mabaya ya internet.
 Gift Msuya kutoka Mkoa wa Vyuo Vikuu akifafanua masula mbali mbali yanayohsu mkoa huo wa vyuo vikuu wakati wa semina ilyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Ramadhani Madabida akitoa mada juu ya mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi katika semina ya siku mbili iliyoshirikisha CCM na CPC kutoka China.
 Katibu Mkuu Msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uenezi akiuliza swali linalohusu ubora wa bidhaa kutoka China wakati wa semina ya siku mbili iliyohushisha CCM na CPC kutoka China.
 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Mboni Mhita akielezea umuhimu wa Umoja wa Vijana wa CCM katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika Hotel ya Courtyard na kushirikisha vyama viwili marafiki CCM na CPC kutoka China.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi kutoka Chama rafiki cha Kikomunisti cha China pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Abdilah Mihewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge.


No comments: