• “Mabadiliko hayatakuja kwa kubadilisha vyama bali ni nia zenu {Mindset) zikifanywa kuwa mpya na mapenzi ya nchi yenu.”
Naibu katibu Mkuu CCM Taifa Mh. Mwigulu Nchemba akiambatana na Uongozi na Marafiki wa CCM tawi la Uingereza wakielekea Leicester
.Baadhi ya Viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la
Uingereza wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa St. Patrick Jijini Leicester
wakisubiri kuwasili kwa Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza Ndugu Maina Owino
akimpokea Naibu Katibu Mkuu wa CCM TAIFA Mh. Mwigulu Nchemba mara alipowasili
kwa ajili ya mkutano na wanachama wa CCM hapa United Kingdom.
Ndugu Abraham Sangiwa wa Itikadi, Siasa na Uenezi
Chama cha Mapinduzi tawi la Uingereza (kulia) wakibadishana mawazo na Ndugu Mwaupete Upete Mwenye suti Nyeusi wa Uchumi
na Fedha CCM tawi la Uingereza nje ya ukumbi wa St. Patrick - Leicester Uingereza kabla ya
Mkutano wa wanachama wote wa CCM hapa UK na Naibu Katibu Mkuu CCM TAIFA
Ndugu Mwigulu Nchemba (MB).
Mtoto wa Katibu wa CCM shina la Jiji la Leicester Uingereza (Ndugu Moses
Kusamba) akimkaribisha Mwigulu Nchemba Kuwasikiliza wanachama wake kwa nyimbo
za kitaifa na chama.
Mkutano wa wanachama ukiendelea kwa wajumbe kuuliza maswali na kutoa
dukuduku zao.
Mwenyekiti wa shina la CCM SOUTHMPTON Ndugu Kapinga Kangoma akiteta na
BEN TV Nje ya Ukumbi wa Mkutano Jijini Leicester – Uingereza.
Watanzania na wana CCM Wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Mh. Nchemba kwa
Makini.
Mshauri wa Rais (Siasa) Ndugu Rajabu Luhwavi akifafanua Jambo ndani mkutano wa
wanachama wa CCM hapa Uingereza.
Katibu wa CCM shina la Birmingham
na Mwenyekiti wa kamati ya Maadili tawi la Uingereza Bi. Lilian Barongo akiwa
pamoja na Mwenyekiti shina la Northmpton Dr. Abdalah Saleh na Bi. Rose Kiputa
Katibu Shina la Cardiff – Wales
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi Taifa na Mbunge wa Iramba Magharibi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba
akisisitiza Jambo katika hotuba yake aliyoitoa hapa nchini Uingereza iliyojaa
mapenzi na Tanzania zaidi ya
Itikadi na kupokelewa vyema na watanzania wengi hapa UK . Posted by: A
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Mbunge wa Iramba Magharibi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama
Katika hali iliyotajwa
kuwa ni ya furaha, kutokana na
changamoto zilizokuwepo siku ya jumamosi jijini Leicester Uingereza, kijana
shupavu na “JEMBE” la kujivunia katika Taifa la Tanzania Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Taifa, na Mbunge wa Ilamba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba
akiambatana na mshauri wa Rais mheshimiwa Rajabu Luhwavi, kwa pamoja waliweza
kutoa majibu ya changamoto nyingi zinazolikabili Taifa kwa watanzania wengi
waliojitokeza katika mkutano mkubwa uliohudhuriwa na watanzania wengi kutoka
maeneo mbali mbali ya Uingereza.
Ujasiri, uwazi na
ukweli wa mambo ya kiutendaji katika taifa letu ndio hasa imekuwa ni chachu na
kivutio kikubwa kwa watanzania wengi waliohudhuria mkutano huo mkubwa jiji
Leicester ambapo Mh. Mwigulu Nchemba aliweza kuweka wazi mengi ambayo serikali
imeweza kuyafanya katika upande wa Elimu, Miundo mbinu na huduma za afya kwa watanzania pia kutoa
kasoro katika maeneo yanayokuwa vikwazo katika kutoa huduma bora.
“Nchi yetu ipo katika
mchakato wa kupata katiba mpya, mojawapo ya mambo ambayo tunayafanyia kazi ni
suala la uraia pacha. Ni pendekezo lililowakirishwa na Chama Cha Mapinduzi
katika baraza zake za uchangiaji maoni ya Katiba mpya. CCM inawajali watanzania
wote hivyo ikaona ni vyema na nyinyi mlioko ughaibuni kupata fursa sawa za
kimaendeleo katika nchi yenu” alisema Mhe. Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Nchemba
aliendelea na kusema kwamba nchi yetu inapita katika kipindi cha mabadiliko.
Idadi ya watanzania imeongezeka kwa kiasi kikubwa na wengi wa ongezeko hili ni vijana
ambao ni watafutaji na wajasiliamali wengi. Kuna haja kubwa kama
chama kubuni taratibu nzuri za kimaendeleo ili kuendana na wimbi hili la
ongezeko la watu.
Mheshimiwa Nchemba kwa
niaba ya Chama Cha Mapinduzi aliwasihi watanzania waishio Uingereza kutumia
upeo (Exposure) waliyonayo katika kulisaidia taifa kupiga hatua zaidi za
kimaendeleo kuliko kuwa na ushabiki wa siasa kama ilivyo kwa baadhi ya
wanasiasa nyumbani na badala yake wawe chemichemi ya mawazo ya kimaendeleo
katika nchi yao .
Watanzania mlioko nje
mna nafasi kubwa ya kuchangia mawazo ya kujenga taifa lenu la Tanzania,
nitawakilisha hoja yenu ya kupatiwa njia ya kuwakilisha mawazo yenu ama jambo
lolote lenye busara na utendaji wa mabadiliko katika nchi yetu ya Tanzania
ili pia mpate fursa ya kuwakilisha maoni na hoja za haja za kuleta mabadiliko. Kutokuwa
na jukwaa lenu la kuwakilisha hoja zenu za kamandeleo ni kosa. Wazo lolote la
kujenga lazima liwakirishwe katika vikao
rasmi kama mchango wa CCM diaspora, liongeza Mheshimiwa Nchemba.
Tengenezeni ajenda
kulingana na ukomavu na upana wenu wa kimawazo ambao mnaupata katika nchi hizi
za Magharibi ambazo zimepiga hatua kubwa za kimaendeleo kutokana na desturi zao
za kuthamini, kujituma na kutenda kazi
zao kwa uadilifu mkubwa kwa mapenzi na nchi zao ili kuchangia utekelezaji wa sera ya chama
katika nchi yetu kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu, miundombinu , sheria
n.k. na mimi naahidi tutatengeneza na kuboresha uwanja mzuri wa mawasiliano
kati yetu aliongeza Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Nchemba pia
alisisitiza upendo na umoja baina ya watanzania na kuwaomba wawe kitu kimoja na
akawataka wana CCM Uingereza kuwa chachu ya kuwaunganisha watanzania wote bila
kujali itikadi za kisiasa na vyama vyao. Mheshimiwa Nchemba pia amekuwa
akikonga nyoyo za watanzania wengi kulingana na utashi na ufahamu wa kujibu
maswali kiufasaha, wazi na kwa uhakika pale alipoulizwa katika mikutano yake
iliyofanyika katika majiji ya Leicester, Northampton
na London
nchini Uingereza.
Katika mkutano
uliofanyika jijini Leicester watanzania wengi waliuliza maswali yanayohusu
Katiba , Utawala wa Sheria wenye haki sawa kwa wote kama ilivyo katika nchi za
kimagharibi, Uraia pacha, Kurugenzi inayoshughulikia masuala ya Diasprora
ambayo badala ya kuwa kiunganishi imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wanadiaspora
kutokana huduma mbovu zenye kutokujali na majivuno kutoka kwa watendaji wake
wakuu, Tunashauri watendaji katika kitengo hiki watokane na wanadiaspora
wenyewe kwani upeo (exposure) wao kiutendaji utaleta ufanisi kuliko ilivyo sasa
hivyo kuleta mchango wao kwa maendeleo ya Taifa. Pia Watanzania hao na wana CCM
wameishauri serikali kubadirisha
taratibu zake za kiajira katika Balozi zetu za nje kwa kuwatumia watanzani
wenyeji wa maeneo hayo ili kupunguza mzigo wa gharama serikali, kuongeza
ufanisi kwani uelewa wa kufanya kazi katika mazingira wanayoishi wanaufahamu
vyema zaidi kuliko kuleta watendaji wote katika Balozi zetu kutoka nyumbani.
Vilevile katika mkutano
uliofanyika jijini Northampton siku ya Jumapili, mengi ya maswali yaliyoulizwa
na watanzania waishio katika jiji hilo ni kama
katika masuala ya usalama wa nchi na raia wake dhidi ya matukio ya
tindikali na majanga ya mabomu kule Arusha, tukio la kigaidi hivi karibuni
nchini Kenya na utayari wa nchi yetu katika kukabiliana na wimbi kama hilo
endapo litatokea nchini kwetu, mikakati ya kupambana na madawa ya kulevya
pamoja na lile gonjwa sugu la rushwa.
Akijibu kwa ufasaha
maswali hayo Mheshimiwa Rajab Luhwavi ambaye anaambatana na Naibu Katibu Mkuu
wa CCM Taifa Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, katika ziara hii, alianza kwa kuwahakikishia
usalama wa taifa Watanzania waliofika katika mkutano huo na kuwaondoa hofu
hiyo. Na kuwajulisha kwamba serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na
uhalifu wa aina hiyo na kwamba taratibu za lazima zinafanyika na hali ni
shwari.
Published by: Abraham Sangiwa
Deputy Secretary Ideology and Publicity
Deputy Secretary Ideology and Publicity
Chama Cha Mapinduzi
Uingereza
(CCMUNITED
KINGDOM )
(CCM
Tarehe 08.10.2013.
2 comments:
Mwigulu Nchemba si kiongozi wa Chama tu bali ni kiongozi wa Taifa. Anazungumzia masuala ya utaifa na kuonyesha njia na ukweli pale palipo sahihi na panapotakiwa kufanyiwa marekebisho. Tuliwaunga mkono watu kama hawa na kuachana na mafisadi ndani ya CCM NCHI ITAENDELEA.
Uzuri wa CCM tofauti na vyama vingine ni chama cha kitaifa chenye kuungwa mkono na watu wa kada na umri mbalimbli. Hata kama uking'oa mafisadi elfu bado hakitetereki kwa maan kina manpower ya kutosha. Mwigulu usiogope mafisadi. Safishasafisha ili nchi izidi kusonga mbele.
Post a Comment