Monday, October 28, 2013

MDAU SIXMUND BEGASHE ALAMBA NONDOZZZ

Mdau Sixmund J. Begashe akifurahi baada ya kulamba nondozz yake ya BA ya Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Sixmund Begashe watatu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimi wenzake wa taaluma ya Mawasiliano ya Umma wakisubiri kudhibitishwa.
Mdau Sixmund akiwa kwenye picha ya pamoja na dada yeke Prof Paula ambae pia ni mkurugenzi wa SPIDER – Sweden. Hadi sasa SPIDER imesha mwaga ma milioni ya Shilingi kuzisaidia taasisi mbali mbali za hapa nchini kikiwemo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mdau Sixmund akimvisha Kofia rafiki yake Bw; Hussein Masimbi alie kuja kumpongeza kwenye maafali ya 25 ya Chuo Kikuu Huria, Bw; Hussein Masimbi ni Mkufunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ( TaSUBa) zamani Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Mdau Sixmund akivishwa shada na Mwanae – Rafiki Mussa Sango (mbunifu wa Jezi za Timu ya Taifa Star) baada ya kuhitimu shaada yake ya Mawasiliano ya Umma katika chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kuli ni Bw; Reina ambae nae alilamba nondozz ya shahada ya kama ya Sixmund.
Wadau kutoka kushoto ni Reina , Kapinga na Sixmund katika picha ya pamoja baada ya kulamba nondozz ya katika chuo kikuu Huria cha Tanzania.

No comments: