Thursday, October 17, 2013

MAZISHI YA NDUGU SANGA NYAMASYEKI ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA TIGO YALIYOYAFANYIKA JIJINI DAR


Safari ya kuelekea makaburini kinondoni imeanza 
Ndugu jamaa na marafiki wakipita karibu na jeneza katika kuuaga mwili wa ndugu sanga nyamasyeki aliyekuwa ni mfanyakazi wa tigo katika ofisi ya huduma kwa wateja kariakoo ambaye alifariki siku ya jumamosi tarehe 12 kwa ugonjwa wa kansa ya damu na kuzikwa leo katika makaburi ya kinondoni alasiri ya leo
wafanyakazi wa tigo nao wakitoA heshima zao za mwisho kwa marehemu
Mmoja wa ndugu wa marehemu akisaidiwa baada ya kushindwa na uchungu mkubwa wa kumpoteza ndugu yake
Umati wa ndugu jamaa marafiki pia wafanyakazi wa tigo wakiwa makaburini kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa marehemu 
       jeneza linaweka taratibu kaburini kwa ajili ya kuzikwa
Marafiki zake wa karibu wa marehemu wakiongozwa na Steven Mtawa wakiweka mataji ya maua juu ya kaburi

mwakilishi toka tigo ndg Edwin Mgoa akiweka maua katika kaburi la ndugu sanga nyamasyeki

Kaka na mdogo wa  marehemu wakisadiwa na mama yao katikati katika kuweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu






baba wa marehemu Dr leonard nyamasyeki na mama mzazi wakiwa katika huzuni katika safari ya miwsho ya mtoto wao mpendwa sanga nyamasyeki





Mchungaji wa kanisa la yehova akitoa neno la mwisho kwa wafiwa na wote waliofika katika mazishi haya alasiri ya leo katika makaburi ya kinondoni jijini dar es salaam
Baba mzazi wa marehemu akitoa shukrani kwa wote waliokuwa pamoja katika kipindi cha ugonjwa na hatimaye kipindi kigumu cha kifo cha mtoto wake mpendwa sanga nyamasyeki

                    MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG inaungana na ndugu jamaa marafiki na wafanyakazi walio katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo kwa kumpoteza mpendwa wao Sanga Nyamasyeki .Mungu alitoa na yeye ndio aliyetwaa jina lake libarikiwe.AMEN
                   Picha zote na Mwanaharakati Mzalendo Blog

No comments: