Gari Maalum lililobeba Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle J),likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam tayari kwa zoezi la kuaga Mwili huo ambao utasafirishwa kwenda Kijijini kwao Tarime,mkoani Mara kwa Mazishi.Marehemu Julius Nyaisangah alikuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD) yeye pamoja na Mikidadi Mahmoud mwanzoni mwa miaka ya 90.
Waanzilishi wengine ni Aboubakary Liongo, Rankim Ramadhan, Flora Nducha,Vicky Msina,Taji Liundi,Charles Hillary na Blandina Munghezi.Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali hapa nchini wakishirikiana kwa pamoja kubeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah (Uncle J) ulipowasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo.
Mmoja wa Wanahabari waliowahi kufanya kazi na Marehemu Julius Nyaisangah,Dkt. Misanya Bingi akiwa amebeba msalaba wenye jina la Marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).Marehemu Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo kushiriki Kuaga Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.Wanaompokea na Wajumbe wa Kamati ya Mazishi (kushoto) ni Aboubakar Liongo na kulia ni Teddy Mapunda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam kuungana na Waombolezaji wengine kuaga Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Julius Nyaisangah pamoja na Waombolezaji mbali mbali,wakati alipowasili viwanjani hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe pia yupo Viwanjani hapa kushirikiana na Waombolezaji mbali mbali kuaga mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.Kushoto ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania,Haidan Ricco.
Wadau mbali mbali wapo viwanjani hapa,Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari,Absaloum Kibanda na katikati ni Muimbaji wa Muziki wa Dansi wa siku nyingi,Mzee Hassan Bichuka.
Waombolezaji.
Wasifu wa Marehemu ukisomwa na Bw. Mapunda.
Wanahabari wakichukua tukio zima la Kuaga.
Wadau mbali mbali wakiwemo waliowahi kufanya kazi na Marehemu,wakishiriki msiba huo.
Mtangazaji Mkonge nchini,Masoud Masoud akiongoza taratibu za Kuaga.
No comments:
Post a Comment