Mwakilishi wa Vodacom mikoa ya
nyanda za juu kusini kati na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa
jukwaa la wahariri nchini Tanzania
Masoud Sanani (kushoto) wakikabidhi msaada wa chakula na vitu mbali
mbali kwa mkuu wa kituo cha yatima cha Huruma Center mjini Iringa
Bi Costansia Chilewa ,msaada uliotolewa jukwaaa la wahariri kwa
ufadhili wa Voda Com Tanzania
Mwakilishi wa Vodacom akimkabidhi
msaada mkuu wa kituo cha yatima cha Huruma Center huku mwakilishi wa
jukwaa la wahariri Bw Masoud Sanani akishuhudia
Baadhi ya wahariri nchini Tanzania na wafanyakazi wa Vodacom wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha
Huruma Center Iringa baada ya kuwakabidhi misaada mbali mbali
iliyotolewa na jukwaa la wahariri kwa ufadhili wa Voda Com Tanzania
Baadhi ya wahariri na wafanyakazi wa
Voda com Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kushusha
msaada wa chakula uliotolewa na jukwaaa hilo na Vodacom Tanzania
Mwakilishi wa jukwaa la wahariri Bw
Masoud Sanani akipongezwa na mkuu wa kituo cha Huruma Center Bi
Costansia Chilewa kwa msaada huo
Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha
Huruma Center Iringa waliopatiwa msaada na jukwaa la wahariri na
Vodacom Tanzania
Magari ya Vodacom yaliyopeleka msaada kituoni hapo
Wahariri wa vyombo vya habari na
wanahabari pamoja na wafanyakazi wa Vodacom wakiondoka kituoni hapo
baada ya kukabidhi msaada wao
Na Francis Godwin Blog
JUKWAA la wahariri nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wamekabidhi msaada wa chakula na vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Huruma Center mjini Iringa.
JUKWAA la wahariri nchini Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania wamekabidhi msaada wa chakula na vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Huruma Center mjini Iringa.
Akikabidhi
msaada huo jana kwa niaba ya jukwaa la wahariri Tanzania mjumbe wa
bodi ya wakurugenzi ya kuwaaa la wahariri nchini Bw Masoud Sanani
alisema kuwa jukwaa la wahariri limetoa msaada huo kwa ufadhili wa
kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania .
Alisema
kuwa imekuwa ni kawaida ya jukwaa hilo la wahariri kwa kushirikiana
na wadau mbali mbali kila mwaka kutembelea na kusaidia watoto
yatima wa eneo ambalo jukwaa hilo litafanya mkutano wake mkuu.
Hivyo
alisema kutokana na mwaka huu mkoa wa Iringa kuteuliwa kuwa
mwenyeji wa mkutano huo wa jukwaa la wahariri ,mkutano
utakaomalizika leo wamelazimika kutembelea kituo hicho na kuungana
na watanzania wengine katika kuwasaidia watoto hao.
Bw
Sanani mbali ya kupongeza jitihada za Voda Com Tanzania kwa
kujitolea kudhamini zoezi hilo bado alisema kuwa kinachofanywa na
wahariri pamoja na wadhamini hao ni sehemu ya kuonyesha kuwa jukumu
la kuwasaidia yatima ni la kila mtanzania kwa nafasi aliyonayo na si
vema jamii kuendelea kuwatenga watoto hao.
Hata
hivyo aliwataka watoto hao yatima kuongeza jitihada katika masomo
na kuacha kusononeka na hali hiyo ya uyatima walionayo kwani
jamii bado itaendelea kuwakumbuka zaidi.
Kwa
upande wake mkuu wa kituo hicho Bi Costansia Chelewa akishukuru Voda
Com na Jukwaa la wahariri kwa msaada huo alisema kuwa msaada huo ni
miongoni mwa misaada mikubwa kutolewa kituoni hapo na kuwa wao kama
kituo wanawapongeza wahariri na Voda com kwa jitihada hizo.
Alisema kuwa kituo hicho kinamilikiwa na kanisa la kiinjili la kirutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa na kina watoto zaidi ya 50 huku moja kati ya mikakati ya kituo ni kuja kuanzisha miradi ya kujitegemea ili kuwafanya watoto hao kuwa na miradi yao.
Kuhusu
changamoto kubwa inayowakabili watoto hao alisema ni pamoja na
walimu kurudisha kituoni mara kwa mara kutokana na michango mbali
mbali ambayo wamekuwa wakitakiwa kulipa shule za msingi.
No comments:
Post a Comment