Monday, October 28, 2013

IBADA YA MSIBA WA MARTHA SHANI DMV

Rev. Nicodemus Hanje akiongoza Ibada ya msiba wa Martha Shani iliyofanyika Jumapili Oct 27, 2013 Greenbelt, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na Watanzania kutoka kila kona na kudhihirisha jinsi gani msiba huu ulivyowagusa wengi na katika historia ya Ubalozi wa Tanzania chini ya Balozi Liberata Mulamula wafanyakazi na maofisa wa Ubalozi huo wamechanga na kununua tiketi tatu za ndege za mume na watoto wa marehemu na kuwawezesha kusafiri kesho Jumatatu Oct 28, 2013 asubuhi na Ethiopia Airline kwenda Tanzania kwa mazishi, mwili wa marehemu utaondoka siku ya Jumaane Oct 29, 2013.
Rev. Nicodemus Hanje akimpa pole mume na watoto wa marehemu kwenye ibada ya kumuombea Martha Shani iliyofanyika Greenbelt, Maryland.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache kuwashukuru Watanzania kwa kuwa kitu kimoja na kuwezesha kufanikisha kuchangisha fedha kipindi cha wiki moja na kuwezesha kumsafirisha marehemu Tanzania kwa mazishi pia Balozi Mulamula aliwakilisha rambi rambi ya Mhe. Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara kwa wafiwa.
Mtoto wa marehemu, Joseph Kassuwi akiwaeleza Watanzania waliofika kwenye Ibada ya mpendwa mama yake maneno aliyoambiwa na mama yake kabla ya pumzi yake ya mwisho alisema mama yake alimuambia amtunze mdogo wake kabla hajamalizia alishindwa kujizuia akaanza kububujikwa na machozi na kufanya watu waliofiak kanisani hapo nao kushindwa kuvumilia.
Wachungaji na maaskofu wakiwaombea familia ya marehemu.
Mume wa marehemu Alex Kassuwi akijaribu kuelezea historia ya yeye na marehemu walivyokutana na jinsi gani walivyokuja Marekani lakini hakuweza kumalizia historia yao baada na yeye kuanza kulia kwa uchungu baada ya kusema yeye na mke wake walikuja Marekani kutafuta maisha baada ya kusema maneno hayo alishindwa kuendelea na kuanza kulia kwa uchungu huku akisaidiwa na Tino Malinda kwenye picha kulia.
DMK kulia akiwatuliza familia ya marehemu waliposhindwa kujizuia na kutokwa na machozi .
Mariam Mtunguja akisoama wasifu wa marehemu kwani yeye alimjua marehemu tangia walipokua na miaka sita. na marehemu alipokuja Marekani na familia yake walifikia nyumbani kwake kabla ya kuanza maisha yao.
Familia ya marehemu wakitoa heshima zao kwa mpendwa wao mwisho wa ibada ya kumuombea mama yao na mke wa Alex Kassuwi.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitoa heshima zake kwa marehemu.
Baada ya watu wote kumaliza kutoa heshima zao kwa marehemu, mume wa marehemu alimvisha pete mpendwa mke wake.
Familia ya marehemu wakiwasha mshumaa kwa pamoja wakati wa chakula cha pamoja.
Mhe. Balozi Liberata Mulaula pamoja na maafisa Ubalozi na Rais wa Watanzania DMV wakifuatilia Ibada

No comments: