Monday, October 28, 2013

BASATA YAIBARIKI MSAMA PROMOTIONS,YAIPA KIBALI CHA KUANDAA TAMASHA LA XMASS

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA)  mapema wiki iliyopita lilikabidhi kibali kwa ajili ya uendeshaji wa Tamasha la Krismasi litakaloendeshwa na kampuni ya Msama Promotions. Tamasha hilo ni muendelezo wa tamasha la Pasaka lililoasisiwa tangu mwaka 2000 likiwa na lengo la kumtukuza na kumtumikia Mungu kupitia nyimbo mbalimbali za waimbaji wa Tanzania na nje ya nchi.


Kabla ya tamasha la Krisimass, Msama alipewa mawazo mengi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wa kutoka  vyombo mbalimbali vya habari. Sababu  za kumtaka  Msama  kuandaa Tamasha la Krisimass ni  kupanua wigo wa kuhubiri Neno la Mungu na kuwapa waamini na wadau wa muziki wa Injili fursa ya kupata burudani kupitia nyimbo za watumishi mbalimbali.   



Kampuni ya Msama inayoandaa matamasha hayo mawili yenye mlengo unaofanana, imedhamiria  kuandaa matamasha hayo mawili ni kufikisha neno la mungu kupitia nyimbo sambamba na mapato yatakayopatikana yatasaidia yatima, walemavu, wajane, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika mazingira hatarishi. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hizo, Alex Msama tamasha la Krisimas litafanyika mikoa mbalimbali ili kuwafikia waumini wengi zaidi lengo likiwa ni kumtukuza na kumuabudu mungu. “Waumini  baada ya kuguswa na neno la mungu katika tamasha la Pasaka,  wamenishauri niandae tamasha la Krismass lengo likiwa ni ibada,” alisema Msama.



Ili kunogesha tamasha  hilo lenye hadhi ya kimataifa,kupitia waimbaji wa Tanzania pia litashirikisha waimbaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kama ilivyo kwenye tamasha la Pasaka siku hiyo waimbaji wote wataimba ‘live’ na hakutakuwa na matumizi ya Play back CD  ama mshindo nyuma. Lengo la Tamasha la  Krismasi kumuabudu Mungu kwa njia ya sifa lakini pia mapato yatakayopatikana yatasaidia wenye uhitaji maalum kama wajane,walemavu, yatima, waathirika wa Ukimwi na wanaoishi katika mazingira hatarishi.



Anasema lengo lingine ni kusherehekea sikukuu ya Krismass na mashabiki na wadau wa muziki wa injili hapa nchini na kufikisha ujumbe wa neno la mungu wenye lengo la kudumisha amani na utulivu hapa nchini.

Anasema pia tamasha hili litashirikisha watumishi wa Mungu kutoka huduma na makanisa mbalimbali kwa ajili ya kuiombea Baraka na amani Taifa laTanzania pamoja na viongozi wao. Aidha Msama alitumia fursa hiyo kuwataka mashibiki na wadau wa muziki wa injil waendelee kufuatilia  ratiba kamili ya tamasha hilo kupitia vyombo mbalimbali vya habari. 



Aidha  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa wa Basata, Nsao Shalua anashauri,  tamasha la krismass mwaka 2013,lianzie mikoani na siku ya kilele ambayo ndio sikukuu yenyewe tukio lifanyike Dar es Salaam.

Anasema kuwe na vitu vya ziada kama akina mama wajasiriamali  kutoka makanisani  na vikundi vingine vitumie fursa hiyo ili kuleta hamasa  ya tamasha husika. Mkuu wa Matukio wa Basata, Kurwijira Maregesi alisema  waimbaji watakaopanda jukwaani mbali ya kuimba nyimbo  zilizozoeleka waimbe pia tungo zenye ujumbe wa  Krisimass ili kudhihirisha uhalisia wa siku yenyewe.  Anasema kabla ya tamasha hilo, Basata itatoa semina kwa waimbaji  ili kuwaweka sawa kabla ya matamasha hayo kuanza.




Maregesi alitumia fursa hiyo kuwaasa waandaaji wa tamasha hilo kulitumia tamasha hilo kama sehemu ya kuwaasa vijana kuachana na mavazi yasiyo ya heshima na matendo mengine yanayomchukiza mungu  na kudumisha maadili ya  muziki wa injili. “Ifike  mahali Tamasha kama la Krismass kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu mienendo mibovu kama mavazi na mengineyo yanayomchukiza mungu.

No comments: