Thursday, September 5, 2013

vurugu bungeni leo dodoma

 
 Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini 
 Wabunge wa CHADEMA wakipambana na Polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo

 Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akisahangaa kuona mapambano kati ya wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni 
 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo 


 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aakiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma leo. hata hivyo   Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafaikiwa kumtoa nje
  Microphone hiyo iling'oka  na polisi wakafaikiwa kumtoa nje

 Mbunge  wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa  na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo
 Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dododma baada ya kuamriwa kufanya  hivyo na Naibu Spika wa  Bunge, Job Ndugai 

 Mbunge wa Mbeya Mjini  akizuiwa na wabunge  wa CHADEMA ili asiambane na polisi, Bungeni Mjini Dodoma leo


13 comments:

Anonymous said...

wapinzani, wamepageuza jumba kubwa kuwa klabu, kila mtu anataka ku endesha mambo kienyeji

Sasa mbowe kaka yangu, watu wamepiga kura 159 against 53 kama kweli wewe unataka demokrasia iendelee kwani huoni kwamba hao 159 ni wengi kuliko 53??? au unataka mwaka 2015 ukipata kubwa CCM wakate.. unajua demokrasia kweli?

Unknown said...

mwaka ujao cheka awe mbunge. ajiri ya ngumi bungen

Anonymous said...

Hili ndio tatizo la kuwatoa watu kwenye bongofleva na kuwapa uheshimiwa, chadema hawana jipya wanatafuta maarufu

Anonymous said...

mwanzoni niliwapenda sana hawa upinzani sasa hivi nipo neutral sipo popote hata sijui wanakotupeleka wanasiasa wa nchi hii ni wapi, cc tunataka kusikia ishu za kujenga, sio vurugu na kuongea hovyo, kutofuata kanuni mara wote mnatoka bungeni, wananchi wenu waliwatuma mkawasemee nyie mnatoka nani awasemee wananchi???
ninchokiona hapa kila mtu anataka kwenda ikulu basi na si maslahi ya taifa.

Anonymous said...

Waheshiwa wabunge tunawaheshimu,tunaomba hadhi ya bunge letu irudishwe! wapi mwalimu Nyerere jamani......

Anonymous said...

nimewachukia kushinda mnavyofikiria hamna maana hata kidogo bunge mmegeuza kama kijiwe cha mateja

Anonymous said...

Daaah inashangaza sana kuona watu walioaminiwa na wananchi kuwa wanaakili timamu leo wabunge na kesho tukiwapa urais c itakuwa balaa mm nawaomba wabunge wawe wastaarabu vinginevyo wananchi uchaguzi ujao tusiwachague hao masela wa vurugu za Disco


Ni mtazamo tu ukimind mwenyewe...........

Anonymous said...

Anonymous 11.31pm

What do you mean kama huna cha kusema kaa kimya alaa!

Anonymous said...

Chadema imepoteza mwelekeo. Imekuwa chama cha wahuni. Wanahitaji mabadiliko ya uongozi. Ni aibu kubwa sana kusababisha vurugu ndani ya bunge. Lawama zote zinatakiwa zimwangukie Mbowe maana jeuri yake ndiyo inayosababisha wafuasi wake walete ukaidi usiokuwa na msingi. Wakina Sugu wanastahili wapewe adhabu kali ili wasirudie ujinga huo tena.

Anonymous said...

KWELI INASIKITISHA BUNGE LETU USTAARABU UMEKOSEKANA GHARAMA TENA ZA KUTENGENEZA MICROPHONE

Anonymous said...

Aibu gani hii! mimi kama mwananchi najisikia aibu sana ... kujivunia utanzania kama enzi zile za mwalimu. The house is goin to the dogs ... no reasoning apart from expressing emotions. Ndugu wabunge jukumu lenu ni kwa watu wenu ... si sera za vyama vyenu.

Anonymous said...

Wote hamfwatilii bunge pia kumbukeni kila kitu kinautaratibu kwani mbowe alitumia nguvu hadi waitwe police? Kukaidi kukaa sio sababu ya askari kuitwa huyo ndugai angetumia busara za kiti chake aidha kumsikiliza la kumwelekeza afanye nini. Asinge waita askari vulugu zisinge kuwepo tukubali kuwa tanzania hatuna demokrasia wengi wape!!!!!

Unknown said...

Kaka unatisha!