Wanaharakati wa mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) wakiwa katika maandamano ya miaka 11 ya tamasha la TGNP nchini na maadhimisho ya miaka 20 ya harakati za ukombozi wa mwanamke
Na Francis Godwin Blog
WANAHARAKATI wa mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) wamefanya maandamano makubwa ya kuazimisha miaka 20 katika kupinga vitendo vya ufisadi pamoja na ukandamizaji wa wanawake .
Huku mtandao huo ukidai kuwa umejipanga kuendeleza mapambano ili kuwawezesha wanawake wa pembezoni kuchukua madaraka ya uongozi katika chaguzi mbali mbali ili kusaidia kuwakomboa wananchi wa pembezoni .
Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Usu Mallya alitoa kauli hiyo leo katika tamasha la 11 la TGNP linaloendelea katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
“Tunashuhudia uporaji wa maliasili zetu yakiwemo madini katika maeneo yetu
…sasa tunataka kuona Raslimali za Taifa ziwanufaishe wananchi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia”
Alisema lazima wanawake na jamii nzima kupambana kuleta mabadiliko ya kweli ya mwanamke na mwanaume pamoja na watoto huku wakitazamwa zaidi wale waliopo pembezoni .
“….Uchambuzi wetu unaonyesha kuwa wanaozidi kubebeshwa mizigo mikubwa zaidi ni wanawake waliopo pembezoni ambao TGNP na washirika wengine tumejipanga kuendelea kuwapigania ili nao waweze kufaidi matunda ya Taifa…
,hivyo lengo letu kuwawezesha wanawake wa pembezoni kuchukua madaraka ili kuweza kuwakomboa wanawake nchini “
Tumefanikiwa topasa sauti kwa kipindi cha miaka 20 sasa katika kupinga vitendo vya ufisadi pamoja na ukandamizaji wa wanawake .
Aidha alisema kuwa harakati ambazo TGNP na washirika wengine wamekuwa wakizifanya ni zimelenga kulikomboa bara la Afrika ,kulikomboa Taifa na kukomboa raslimali za taifa zisiwanufaishe watu wachache .
Kwani alisema kuwa TGNP wameanza kupasa sauti katika kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana kwa watu wote na kuepuka mfumo dume na kandamizi kwa wanawake na watoto toka mtandao huo ulipoanzishwa mwaka 1993.
Alisema miaka 20 iliyopita Suala la jinsia lilikuwa ni kama hadhithi na suala la mfumo dume lilikuwa halizungumzwi kabisa ila kwa sasa kila mmoja anatambua na kuzungumzia suala hilo masuala ya jinsia na mfumo dume .
Kuhusu kuendelea kukithiri kwa rushwa za ngono katika maeneo ya kazi Mallya alisema kuwa rushwa ya ngono ni chanzo cha kuendelea kumnyanyasa mtoto wa kike nchini na kuwa bado suala hilo ni kikwazo na wao kama wanaharakati wataendelea kupaza sauti na kupambana na vitendo vya rushwa za ngono .
“Bajeti ya kijinsia lazima iweze kuanzishwa ili kuwezesha haki na usawa kati ya wanaume na wanawake inakuwepo kama njia ya kuyawezesha makundi yote kunufaika na raslimali ya Taifa “.
Wakati huo huo washiriki wa maandamano na tamasha hilo wameitaka serikali kuchukua hatua kali kuwawajibisha wale wote wanaoendesha biashara ya madawa ya kulevya ambayo yameendelea kulichafua Taifa na hata kuwafanya vijana wengi kupoteza maisha kwa utumiaji wa madawa hayo na kuacha mateso kwa wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment