Friday, September 27, 2013

TAMASHA LA KIMATAIFA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO 2013 LAZIDI KUPENDEZA

 Kiongozi wa Kundi la Ngoma za asili la Albino Revolution,akiimba moja ya nyimbo zao za kuhamasisha amani pamoja na kuwasali watu wenye Ulemavu,wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Chuo Kukuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.Tamasha hilo lilaloonekana kuwa na wapenzi wengi kutoka sehemu mbali mbali,linatarajiwa kumalizika Septemba 28,2013.
Mmoja wa Wasanii wa Kundi la Ngoma za asili la Albino Revolution akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma hizo kwa namna yake.
 Burudani imekolea huku shangwe zikisikika ukumbi mzima.
 Umoja ni Nguvu.
 Hii namna ya kumaliza burudani kwa Wasanii hawa.
 Pichani ni kivuli cha Msanii wa Maigizo wa Kundi la Mapoloni Cultural Group aliekuwa akiigiza Jukwaani wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Chuo Kikuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.
 Wasanii wa Maigizo na Ngoma za asili wa Kundi la Mapoloni,wakionyesha umahiri wao wa kuigiza Jukwaani wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Chuo Kikuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.
 Mwanadada akijiamwayamwaya jukwaani kwa raha zake.
 Maigizo yakiendelea.
 Wachezaji wa Ngoma za Asili wakionyesha Umahizi wao jukwaani.

No comments: