Na Mwandishi Wetu
Sekta ya pamba nchini ina uwezo wa kuwakwamua wakulima wa pamba katika dimbwi la umaskini endapo serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wataweza kusaidia uwepo kilimo cha mkataba nchini.
Akiongea na vyombo vya habari hivi karibu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Gabriel Mwalo, alisema kuna faida nyingi katika kilimo cha mkataba lakini kukosekana kwa usimamiaji mzuri pamoja na ukosefu wa uungwaji mkono wa kutosha kutoka Serikalini kunawafanya wawekezaji kutochangia fedha nyingi zinazohitajika katika mfumo.
Sasa wakati umefika kwa Serikali kuyaangalia matatizo yanayokwamisha kilimo cha mkataba na mkazo uwekwe kwenye uzalishaji wa pamba pasiwepo ucheleweshaji wa utekelezaji wa sera ya Serikali,” Bw. Mwalo alisema.
"Mfumo wa kilimo cha mkataba (ambao umesimamishwa) lazima uboreshwe ili kuwawezesha wakulima kuongeza tija.
“Sekta ya pamba, kupitia msaada wa Serikali, wasindikaji na wawekezaji, ina fursa ya kufanya maendeleo kwa wakulima kwa ujumla na inaendana vizuri na ahadi ya Serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Kama Serikali, inapaswa kuingilia kati na kuweka mazingira yatakayohakikisha kunakuwepo na maendeleo na mkulima kuwa endelevu pamoja na kilimo cha mkataba kwa ujumla.
"Wawekezaji wakubwa wanahitaji wakulima wanaoweza kuwasambazia pamba zitakazotumika kwenye vinu vyao, huku wakulima nao wanahitaji wawekezaji kuwapa mitaji kuendesha mashamba yao na kuongeza mavuno.
"Kama Serikali inaingilia kati na kusimamia vizuri kilimo cha mkataba, itakuwa ni hali ya ushindi,” Bw. Mwalo alisisitiza.
Aliongeza kusema kwamba hivi leo ekari moja huzalisha kuanzia kilo 250 mpaka 300 za pamba na kama kilimo cha mkataba kitaungwa mkono ipasavyo na Serikali na matatizo machache ya msingi kushugulikiwa, panaweza pakawepo na mavuni kuanzia kilo 1200 mpaka 1500k kwa ekari moja.
Afisa huyo aliyataja baadhi ya matatizo kama vile mbegu za pamba zisizothitishwa, wakulima kutumia mbolea kidogo au kutotumia mbolea kabisa pamoja na kuwepo dawa kidogo za kuulia wadudu na ukosenekaji wa zana za kilimo kama sababu kubwa zinazofanya mavuno ya pamba kuwa machache nchini.
Kuna mahitaji makubwa ya zao la pamba duniani, kama takwimu za hivi karibuni kutoka Benki Kuu Tanzania ni za kuzingatiwa, thamani ya mauzo ya bidhaa za asili nje ya nchi yaliongezeka kwa sababu ya ongezeko la uuzaji wa pamba nje ya nchi ikiambatana na hali nzuri ya hewa sehemu za upandaji pamoja na bei nzuri iliyokuwa ikitolewa miaka iliyopita.
Ripoti ya marejeo ya uchumi ya BoT inaonesha kwamba mwishoni mwa Juni mwaka huu thamani ya mauzo ya nje ya pamba yalikuwa Shilingi bilioni 254.4 (dola milioni 159.3).
Pamoja na Tanzania kuwa mzalishaji mkuu wa pamba inayoshika nafasi ya nne Afrika baada ya Mali, Burkina Faso na Egypt, kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo, juhudi zaidi kwa Serikali zinahitajika kutekelezwa ili kufikia lengo laTCB la kupata kilo 1500 kwa ekari moja.
"Pamba bado inaweza ikawa zao la biashara linaloweza kuiingizia Tanzania fedha nyingi Tanzania ingawa kiwango cha mavuno kimedumaa kwa kiasi kikubwa kwa miaka mingi na kuna haja kubwa ya kuboreshwa,” alisema.
Uzalishaji wa pamba Tanzania uliongezeka kwa asilimia 57 mwaka jana kutoka tani 225,000 zilizozalishwa 2011, na hiyo imetokana na kusaidiwa na kilimo cha mkataba nchini kufutatia miaka mitatu ya mpango wa majaribio kaskazini magharibi ya Mkoa wa Mara.
Chini ya mfumo huo, wakulima walikubaliana na wanunuzi kusambaza viwango maalumu na kuzingatia ubora wa zao hilo, na wakulipa walipata fursa ya kupata mikopo ya pembejeo kama vile dawa za kuulia wadudu, Mwalo alisema.
Hali hiyo inataka kuwepo na haja ya mawakala na wakopeshaji wa ndani kurahisisha mahusiano katika ya wazalishaji na wanunuzi, alisema he said.
Kama Serikali itachukua hatua za haraka kuunga mkono kilimo cha mkataba, mauzo ya pamba nje ya nchi huenda yakaongezeka na kuwaingizia wakulipa mapato mazuri.
Msimu uliopita ulishuhudia wakulima wakiingiza shilingi 700 kwa kila kilo ya pamba.
Septemba mwaka jana, serikali ilisisiza kwamba wakulima waingie katika kilimo cha mkataba, kwani ni mfumo ulio bora zaidi katika kuongeza uzalishaji wa pamba.
Sekta ndogo ya pamba Tanzania, ambayo inaajiri watu milioni 14, kiasi cha asilimia 40 ya idadi ya watu nchini, huenda ikafa kabisa, au Serikali ikitaka ichukue hatua za hataka kuokoa hali.
Jana, mkaguzi wa pamba, Igore Maanonga, aliiambia 'Citizen' wakulima wengi walishawishika au kudanganywa na wafanyabiashara wasio waaminifu katika dhana kwamba kilimo cha mkataba kinapunguza mapato ya wakulima.
"Wengi wa wafanyabiashara hawa wanaona kwamba watapoteza biashara kama wakulima wataingia katika kilimo cha mkataba na wanaamua kusambaza propaganda mbaya kwa wakulima,” alisema.
Jana, mkulima mmoja wa pamba na mkazi wa kijiji cha Kinyambwita, kata ya Ubutu mkoani Mwanza, Magore Masungura, aliliambia gazeti la 'Citizen' kwamba kilimo cha mkataba kimebadili maisha yake.
"Baada ya kuingia kilimo cha mkataba mavuno yangu ya pamba yaliongezeka kutoka kilo 500 mwaka 2011 hadi kilo 2980 mwaka 2012 katika shamba langu la ekari mbili," anasema.
Kutokana na mafanikio yake - Magore anasema ameweza kununua nyumba mbili kubwa na pikipiki.
Hivi leo uzalishaji wa pamba umeongezeka zaidi hadi kufikia tani 2.981 kwa ekari moja,ambapo aliweza kuuza kilo moja ya pamba kwa shilingi 700.
“Kilimo cha mkataba ndo ufumbuzi wa kilimo cha pamba nchini. Kwa ukweli kilimo cha mkataba ni chachu ya maendeleo ya wakulima wa pamba nchini Tanzania,” Bw. Magore anasema.
Ameishauri Serikali ya Tanzania kuwapa wakulima pembejeo zaidi ili waweze kufaidika zaidi kupitia mfumo mpya wa kilimo cha mkataba ambao tayari umekwisha badilisha maisha ya wakulima wengi.
Magore anasema zaidi kwamba tatizo la wakulima kuondolewa kwenye mfumo mpya wa kilimo ni propaganda ambayo inaendeshwa na wanasiasa, wafanyabiashara kwa ndiyo hao wanaomiliki maduka ya pembejeo za kilimo.
Zaidi ya makampuni 40 ya usindikaji na zaidi ya watu milioni 14 walioajiriwa katika sekta ndogo ya pamba, wakati umefika sasa kwa serikali kuunga mkono kwa ukamilifu kilimo cha mkataba,” alihitimisha kusema Bw. Gabriel.
No comments:
Post a Comment