Sunday, September 1, 2013

REDD'S MISS PHOTOGENIC TANZANIA 2013 KUJULIKANA LEO

WASHIRIKI wa shindano la Redd's Miss Tanzania leo watapata fursa ya kumjua mrembo wa kwanza kuingia katika hatua ya Nusu fainali ya Shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 wakati mrembo mmoja kati ya wanyange hao 30 atakapotajwa mshindi wa Miss Photogenic 2013.

Shindano hilo no moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusufainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao.

Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.

Akizungumza na Father Kidevu Blog hii leo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.

Mshindi anataraji kutangazwa leo jioni katika hoteli ya Giraffe Ocean View na kujipatia tiketi hiyo.

Taji la Redd's Miss Tanania Photogenic  linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012. Wafuatao ndio warembo watakao wania taji hilo hii leo.

 ESHYA RASHID
JANETH AWET
 HAPPINESS WATIMANYWA
CLARA BAYO
DORICE MOLLEL
 LATIFA MOHAMED
SALSHA ISDORY
 PRISCA PAUL
 LUCY TOMEKA
SEVERINA LWINGA
 SABRINA JUMA
 MIRIAM MANYANGA
LINA ALLAN
 LUCY JAMES

GLORY STEPHEN
 NEEMA SHAYO
 ALICE ISAACK
 SARAH PAUL
 PHILLIOS LEMI

NANCY MOSHI
 JACLINE LUVANDA
 DIANA LAIZER
 LUCY CHARLES
 SVETLANA NYAMEYO

NARIETHA BONIFACE
 MARY CHEMPONDA
 NICE JACK HERMAN
ANASTAZIA DONALD
 NEEMA MALITI
ELIZABETH PERTY

No comments: