Kazi imefanyika usiku mkubwa chini ya usimamizi wa askari polisi.
Sehemu ya mauongio ya maji katika njia kuu ya maji iliyopita ndani ya eneo hilo.
Ofisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Dorah
Killo akiangalia moja ya tanki la ardhini ambalo limekuwa likitumika
kuhifadhia maji ambayo yameunganishwa kwa wizi kwa ajili ya kunyweshea
na kuogeshea Nguruwe.
Sehemu ambako hujuma ya maji imekuwa ikifanyika katika moja ya eneo la
kufugia Nguruwe katika kata ya Korongoni.
Fundi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi.MUWSA akichimba
eneo ambalo kuna bomba la maji lililounganishwa kwa wizi katika
miuondo mbinu ya mamlaka hiyo.
Nguruwe zaidi ya 70 wanaofugwa katika eneo hilo ambao maji
yaliyounganishwa kwa njia ya wizi yamekuwa yakitumika kuwaogesha na
kunyweshea.Shoto ni ofisa uhusiano msaidizi wa MUWSA ,Florah Stanley.
Mafundi wakiendelea kufukua bomba lililounganishwa kwa wizi.
Baada ya kusimama muda mrefu baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudio
tukio hilo la kutafuta maungio ya maji walilazimika kunywa maji yale
yale yaliyoungwa kwa wizi.
Sehemu ya mauongio ya maji katika njia kuu ya maji iliyopita ndani ya eneo hilo.
Baada ya kusimama muda mrefu baadhi ya watu waliokuwa wakishuhudio
tukio hilo la kutafuta maungio ya maji walilazimika kunywa maji yale
yale yaliyoungwa kwa wizi.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
SIKU chache baada ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi
(MUWSA) kubaini kufanyiwa hujuma ya wizi wa maji katika mitandao
yake,mamlaka hiyo sasa imeanzisha operesheni isiyo na kikomo huku
ikiwatumia askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) kusaka
wezi hao nyumba kwa nyumba.
Operesheni hiyo imeanza hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya mji
wa Moshi hususani yale yenye viwanda na maeneo yanayokaliwa na watu wa
kipato cha juu ambayo yanatajwa kujihusisha na wizi wa maji kwa
kujiunganishia kinyume cha sheria.
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,John
Ndetiko alisema operesheni hiyo imeanza wakati huu ambao kuna upungufu
mkubwa wa maji hivyo ufuatiliaji utafanyika katika eneo moja hadi
jingine ili kuwabaini wezi wa maji.
“Zoezi hili litakuwa ni endelevu kabisa katika kipindi chote cha uhai
wa mamlaka ya maji taka na maji safi mjini Moshi na tumeamua kuianza
sasa kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji katika maeneo
mengi kwa hiyo tutafanya ufuatiliaji katika eneo moja baada ya na
jingine ili kuwabaini wanaofanya hujuma hiyo na kuwapeleka kwenye
vyombo vya sheria.”alisema Ndetiko.
Akizungumzia kwa nini wameamua kuwatumia askari polisi wa kikosi cha
kutuliza ghasia(FFU)Ofisa uhusiano wa mamlaka hiyo Dorah Kilo alisema
sheria za mamlaka zinaruhusu maofisa wake kuingia sehemu yoyote kwa
mtu anayetumia maji ama hatumii maji kwa lengo la kukagua miundo mbinu
isifanyiwe hujuma.
Alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya kiusalama kutokana na maeneo
mengine watumiaji wa maji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kufungua
milango yao licha ya kujitambulisha kwao hali inayopelekea kutumia
jeshi la polisi pamoja na viongozi wa mitaa husika.
“Mara nyingi tunatangulia sisi wenyewe katika eneo husika,tunakuja
kirafiki tunazungumza ili kuweza kutambua matatizo yako na kasha
kuchukuliwa hatua, lakini unapokuwa unaleta ugumu wa kutoa ushirikiano
pale ndipo tunalazimika kuwaagiza askari polisi kuja kuongeza
nguvu.”alisema Killo.
Alitoa wito kwa wakazi wa mji wa Moshi na maeneo mengine
yanayosimamiwa na mamlaka hiyo kutoa taarifa za hujuma ya maji katika
maeneo yao na kwamba atakayotoa taarifa sahihi ya wizi huo atazawadiwa
na mamlaka hiyo kiasi cha fedha ambazo hata hivyo hakukitaja.
No comments:
Post a Comment