KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Unguja , ambapo alimwakilisha Ridhwan Kikwete .
VIONGOZI mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliohudhuria mkutano wa hadhara katika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza mgeni Rasmi Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba (hayupo pichani) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka.
WANACHAMA wapya 126 waliojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo 61 walitoka chama cha CUF na 65 wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha uongozi wa fedha Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
MMOJA wa Wanachama 61 waliotoka Chama cha CUF Jimbo la Chwaka, Lailat Abdalla akielezea sababu za kutoka hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM) mbele ya Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka (CCM) Issa Haji Ussi (Gavu) akitoa salamu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya chuo cha uongozi wa fedha Chwaka, kulia mgeni rasmi katika mkutano huo, Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba.
KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba (kulia) akimkabidhi seti za jezi na mipira Katibu CCM Wadi ya Dunga, Maryam Kondo Mwadini kwa niaba ya timu za mpira wa miguu zilizopo katika wadi yake, makabidhiano hayo yalifanyika katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Chwaka Wilaya ya kati Unguja.(Picha na Haroub Hussein).
No comments:
Post a Comment