Thursday, September 19, 2013

Mavazi na Urembo kutoka kwa Mdau Freddy Macha

-Na Freddy Macha
LOGO -fashion Sept 7- by Sara Abood 
  Mchoro wa shughuli uliobuniwa na Sara Abood. 

Wabunifu mavazi wanne toka Tanzania walioshiriki maonesho ya mavazi Ubalozi wetu London Jumamosi Septemba Saba wamechaguliwa kuingia dimba la kimataifa London Fashion Week, Februari mwakani. Wasanii hao waliopewa nafasi ya kujitangaza kupitia jitihada za Jumuiya ya Wanawake Uingereza (TAWA) ukishirikiana na Ubalozi ni mseto wa wafanyabiashara wakongwe na vijana wanaoanza fani hii ya urembo.Mama Joyce Kallaghe-pic by Felipe Camacho 
  Mama Joyce Kallaghe, ni mtangazaji mzuri wa mavazi ya Kitanzania ughaibuni. Picha na Felipe Camacho. Akifungua shughuli hii, mkewe Balozi, Mama Joyce Kallaghe alikumbusha hii ni nafasi nzuri kwetu. “ London Fashion Week” ni tafrija maarufu inayofanyika sambamba Paris, New York, Milan mwezi Februari na Septemba kila mwaka toka 1984. Mbali na msaada wa TAWA na Ubalozi, mwekezaji mkuu wa shughuli hii ni British Council- shirika linaloendeleza vipaji nchi zaidi ya 100 duniani kwa miaka 75 sasa. Mada ya maonesho iliitwa “Fahari Passion 2013” na mchoro wake uliobuniwa na Bi. Sara Abood unaonyesha uso wa mwanamke na rangi za bendera ya taifa.
Khanga dress tight 
Khanga inavyojigamba na kupendeza. Picha na Abubakar Faraji

Dhamira hii ya “kujivunia chako” ilionekana katika mseto wa nguo fupi, magauni makubwa, sketi, mitandio, lubega, vijikaptula, vijikoti, visibau, nguo za heshima au za kubana, mabega wazi na yaliyozibwa, za starehe au faragha nk. Vyote havikukosa vazi la kanga ama kitenge, ingawa vitambaa vya aina nyingine kama batiki pia vilitumika.Hand on Djembe 
Ngoma za Kitanzania pia zilipigwa Wanawake wazuri wazuri wenye haiba, wajihi na maumbo ya kila namna waliotembeza mavazi (“models”)walichanganya Wazungu, Wahindi na Waafrika, sura mahusi za jijini London. Wabunifu hao wanne walihojiwa na Bwana Abubakar Faraji aliyekuwa mwendesha shughul (MC) usiku huo uliofana sana.Lubega 
Lubega la Kimasai. Picha ya A Faraji. Hamida Ramadhani wa “All Things African” alieleza : “ Nnaunga mkono jumuiya za Watanzania wasiojiweza kwa kuuza kazi zao za mitindo ya Kiafrika, mapambo ya vito, viatu na kazi za sanaa za mikono.” Dhana kuu ya Bi Jaquiliene Majebelle ni mavazi ya mwanamke na “vyote vinavyomfanya apendezeshe umaridadi wa kike, mapambo ya kifalme, uchangamfu, nguvu na ukunjufu.”Khanga as a skirt 
 Basia Hellela ( House of Wellu) alisema azma yake ni “kubuni mavazi ya kike, ya kihafari, ila rahisi kuvaa pasina noma yeyote ile.” Mkewe mshoni maarufu, Manju Masita, anayesoma Uingereza, Mija Sayi alianza kupenda mavazi toka akiwa mtoto mdogo wa miaka sita,na anaamini “alizaliwa kuleta mabadiliko katika jamii na amani duniani.”Casual and 

attractive 
Mwanamke ni hulka...Khanga in flowers 
Khanga ina uwezo wa kumpendeza mwanamke yeyote...

No comments: