Miaka miwili ya Mpango wa kupeleka
madaktari bingwa vijijini unaoratibiwa na
Mpango wa Afya- KNCU (Juni 2011 mpaka Juni 2013)
Utangulizi
Mpango wa Afya KNCU ulianzishwa
Aprili 2011, ukiwa na lengo kuu la kuhakikisha wakulima wa kahawa mkoani
Kilimanjaro wanapata huduma ya Afya wakati wowote wanapoihitaji. Mpango huu
unasimamiwa kwa karibu na PharmAccess, ambao kupitia serikali ya Uholanzi ndio
wadhamini wakuu wa mradi. KNCU wanashirikiana kuhakikisha kuwa wanachama wao
wanashiriki kwa wingi na wanapata huduma stahiki.
Mpaka sasa, jumla ya watu 16,000
ambao ni wakulima na wategemezi wao wamejiunga na mpango huu. Wanachama hawa
wanapata huduma katika vituo 20 vya Afya vilivyoteuliwa na mpango wa afya – KNCU.
Mpango
wa kupeleka madaktari bingwa vijijini
Mara baada ya mpango wa Afya KNCU
kuanzishwa, PharmAccess kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa KCMC walianza
kutoa huduma ya madaktari bingwa kwenda kutoa huduma vijijini. Utaratibu huu
ulianza Juni 2011. Sababu kuu zilizopelekea huduma hizi vijijini ni kama
zifuatazo;
i.
Kuwajengea uwezo watoa huduma wa Afya
walioko vijijini, kwa njia ya kufundisha kwa vitendo (clinical
mentoring),kuendesha semina kila wanapowatembelea na kupitia mafaili ya
wagonjwa ili kuelekeza matibabu sahihi ya wagonjwa.
ii.
Kutoa matibabu ya magonjwa sugu (mf.
kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya mifupa kama gout n.k) kwa watu
wanaoishi vijijini (wanachama na wasio wanachama wa mpango wa Afya KNCU)
iii.
Kuendesha kliniki kwa watoto wenye magonjwa
ambayo yameshindwa kugundulika au kutibika na madaktari wa zahanati (mf.
Cerebral palsy, kifafa n.k)
Wanakijiji wanalazimika kulipia
angalau sh. 3,000 kuweza kumuona daktari kama sio mwanachama wa mfuko wa afya
KNCU, na bila kulipia gharama yoyote ikiwa yeye ni mwanachama.
Baada ya kuendeshwa kwa mafanikio
kwa kipindi cha miaka miwili, madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi
waliongezwa kwenye mpango, ambako huenda kutoa mafunzo, kuwapima na kuwashauri
wajawazito na kutibu magonjwa ya kawaida ya wanawake.
Mafanikio
yaliyopatikana
Kwa ujumla, wagonjwa 1,887 wamepewa
matibabu na madaktari bingwa katika mahudhurio
203 kwa kipindi cha miaka miwili, kama jedwali la chini linavyoonyesha
|
June to Dec 2011
|
Jan to Dec 2012
|
Jan to June 2013
|
|||
Speciality
|
Visits
|
Patients
seen
|
Visits
|
Patients
seen
|
Visits
|
Patients
seen
|
Paediatrics
|
26
|
72
|
39
|
308
|
18
|
208
|
Physician
|
34
|
123
|
60
|
777
|
23
|
375
|
Gynaecologists
|
0
|
0
|
0
|
0
|
3
|
24
|
Total
|
60
|
195
|
99
|
1085
|
44
|
607
|
Faida
zilizopatikana
Licha ya faida
nyingi za moja kwa moja na zisizoonekana moja kwa moja, taarifa hii
itaorodhesha faida chache
i.
Wanakijiji wenye magonjwa sugu wamepata
huduma kwa gharama nafuu bila kulazimika kuja mjini kwa matibabu, hivyo
kuwapunguzia gharama na usumbufu
ii.
Watu wengi wamegunduliwa na matatizo
(yaliyokuwa hatua za awali) ambayo yalishindwa kugundulika katika zahanati. Mf.
Ugonjwa wa ini, cerebral palsy etc.
iii.
Baadhi ya wagonjwa waliokuwa na matatizo
yaliyoshindikana, wamepata rufaa kuja KCMC kwa matibabu zaidi. Kwa mwaka 2012,
jumla ya wagonjwa 66 walipewa rufaa.
iv.
Mafunzo ya matibabu kwa nadharia na vitendo
yametolewa kwa madaktari wa zahanati vijijini.
v.
Kumekuwa na mtandao kati ya madaktari
bingwa wa KCMC na madaktari wa vijijini, ambapo wamekuwa wakiwasiliana kwa simu
pale daktari wa kijijini anapohitaji ushauri wa kutoa matibabu.
Changamoto
i.
Gharama za kuwapeleka madaktari bingwa ni
kubwa.
ii.
Upungufu wa madaktari bingwa, hasa wakati
huu ambapo vituo vya mradi vinaongezeka.
iii.
Ufahamu wa wanakijiji kuhusu ujio wa
madaktari wa KCMC.
iv.
Mahudhurio ya wagonjwa wa kawaida,
wasiohitaji matibabu ya daktari bingwa.
Dondoo kwa
Wahariri na Bloggers:
- Mpango
wa Afya wa KNCU ni rafiki, hutoa huduma za afya ya msingi, pamoja na
magonjwa sugu katika kituo kilicho karibu na pale mwanachama anapoishi.
- wamama wengi wamekuwa awakipoteza uhai
wao na watoto wao wakati wa kujifungua kutokana na matatizo ya uzazi.
Mpango wa Afya wa KNCU katika kulinda maisha ya mama na motto inatoa
huduma ya salama ya kujifungua katika vituo vya msingi, na rufaa wilayani
na hata KCMC pale inapobidi.
- Mpaka
sasa kinamama 21 wamepata huduma hii chini ya mpango wa afya wa KNCU,
baadhi ya ni Mama Krismata kutoka chama cha msingi Marangu Marangu
Magharibi, Mama Flaviana Mboya kutoka
chama cha msingi Marangu Mashariki, Grace Gilbert Lema kutoka chama
cha msingi Machame Wari, Hellen William Lyimo kutoka chama cha msingi
Kilema South, Etyefose Noel Massawe kutoka chama cha msingi Masama Mula,
Haikael Jackson kutoka chama cha msingi Marangu Mashariki na Anna Paul
Urassa kutoka chama cha msingi Mrimbo Uuwo.
Uboreshaji huduma.
- Mpango
wa Afya wa KNCU kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO)
unaendelea na juhudi za kuboresha huduma katika vituo vinavyotoa huduma
katika mpango huu chini ya mpango wa huduma salama (SafeCare).
- Vituo
hivi ni zahanati za Mango, Mrimbo Uuwo,
Mamba Mboni, Umbwe, Lole, Rauya, Mbahe, Mango , Makomu, Sanya Juu, Mashati na Lemira vituo vya
afya vya Masama Government, Masama Lutheran na Mwika Msae. Pia Hospitali
za Marangu, Kilema, Kibosho na Ngoyoni.
- Vituo vilivyotajwa hapo juu vimefanyiwa ukarabati kabla ya wanachama
wa Mpango wa Afya wa KNCU kuanza kupata huduma. Mara nyingi ukarabati
hugharimu si chini ya Tshs milioni 50 kwa kituo kwa wastani.
- Zahanati
ya Rauya, Mrimbo Uuwo, Lole na kituo cha Afya cha Mwika Msae vimefuzu na
kupata daraja la hatua ya kwanza ya uboreshaji huduma chini ya mpango wa
huduma salama (SafeCare).
- Mafunzo
mbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma za kitabibu yanaendelea
kutolewa na wataalamu wa PharmAccess na MicroEnsure.
- Tathmini
mbalimbali za utoaji huduma na mtazamo wa huduma hizo zinaendelewa
kukusanywa na huingizwa moja kwa moja kwenye mpango wa kuboresha huduma.
- Wataalamu
kutoka KCMC wanatembelea vituo vilivyopo kwenye mpango wa Afya wa KNCU
walau mara mbili kwa mwezi. Kwa mfano kwa mwaka 2012 madaktari wataalamu
kutoka KCMC walitembelea vituo vilivyopo katika mpango wa Afya wa KNCU
zaidi ya mara 99.
No comments:
Post a Comment