Jackson M. Kalikumtima
Mwenyekiti Mtendaji
|
Shindano la Tanzania Top Model limeanzishwa
ili kuziba ombwe lililoko la kuwatafuta,
kuwatayarisha na kuwatafutia mikataba wanamitindo wa kitanzania ambao ndoto
zao zimekuwa ni kufanikiwa na kuwa wanamitindo wa Kitaifa na Kimataifa. Ni
shindano litakalo wajenga na kuwafanya wajiamini na waaminiwe kwa kazi
mbalimbali. Hiki kitakuwa ni kichocheo kingine cha kuitangaza nchi yetu katika
mavazi na sanaa nyingine kimataifa na kuwa chimbuko la nyota nyingine katika
dunia ya Wanamitindo hapa nchini.
Mashindano
ya kumtafuta Tanzania Top Model si mashindano ya kawaida kama tulivyo zoea
mashindano ya kuwakutanisha Washiriki na kupima Mshiriki aliye bora tu kuliko
wenzake, bali ni Mashindano ya kumtafuta Mwanamitindo bora tena wa Mfano hapa
nchini. Haya ni mashindano yatakayo ruhusu Jamii/ Wananchi/ Wadau kushiriki
kuchagua mshindi kwa kiwango Fulani.
Judgement au Maamuzi wa nani ashinde
shindano hili yatafanywa na makundi manne tofauti ambapo wananchi watachagua
mshindi kwa kupiga kura kwa ujumbe mfupi kupitia simu zao za viganjani na
kupitia kwenye mtandao (tunaamini vyombo vya habari mtatusaidia sana katika
hili kwa kuhamasisha wananchi wengi iwezekanavyo wapige kura zao na kuchagua
mshindi).
Maamuzi yao yatakuwa ni kwa asilimia 20. Waalimu, Washauri nasaha,
Wakufunzi, Wawezeshaji watakao kuwa mafunzo mbalimbali wakati wa kambi ya
Washiriki watakuwa na maamuzi ya mshindi kwa asilimia 15. Matron na watu wa
kambi walinzi, wafanya usafi watakuwa na maamuzi kwa asilimia 5 ya alama zote.
Asilimia 60 zilizobaki zitatolewa na Majaji watakaofanya kazi hiyo kwenye
onyesho la mwisho.
Mashindano
haya, katika ngazi ya fainali yataendeshwa kama kipindi cha kwenye Televisheni
(Reality TV Show) na kurushwa katika kituo kimojawapo hapa nchini kuanzia
Novemba moja hadi siku ya Fainali ya Onesho hilo ambalo litakuwa linakwenda
sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania kila mwaka. Kwa kuyafanya mashindano
haya kuwa sehemu ya kipindi cha televisheni, tutakuwa tunawapa nafasi wananchi
na wadau wa Tanzania Top Model waweze kuona na kumpigia kura mshiriki ambao
wanadhani anafaa kuwa mshindi na kuwawakilisha katika mashindano ya kimataifa
ya Top Model of the World. Kwa kuwarusha kwenye kipindi cha Televisheni kwa
muda mrefu kiasi hiki, tutakuwa tunawajengea nafasi washiriki wetu ya kuwa watu
maarufu na kuwafanya wakubalike kwenye jamii na waweze kuajirika.
Kwa kuanzisha
shindano hili, Kampuni ya Tanzania Top Model Agency Limited ina malengo makuu ambayo
ni pamoja na Kuenzi, kukuza na
kuendeleza vipaji vya wasanii ambao kwa namna mbalimbali watajihusisha na
shindano hili ili kuwafanya wajitegemee katika maisha na kuwa na uhakika wa
maisha bora. Pamoja na nilichotaja malengo mengine yatakuwa ni
1 Kuwatafuta, kuwainua wanamitindo chipukizi
wenye vipaji na wasio na majina
katika fani hii na kuwafanya wajulikane ndani na nje ya nchi, huku tukiwajengea
uwezo wa kujiamnini kwa kile wanachokifanya.
2. Kutoa ushauri wa Kitaalamu unaohusu masuala
ya fani mbali mbali ili kuwawezesha washiriki waweze kukubalika katika soko la
ajira kwenye mitindo, maonyesho ya mavazi au kazi nyinginezo.
3. Kumtafuta Mwakilishi wa Tanzania katika
Mashindano Top Model of the World.
4. Kuenzi,
kuhifadhi na kuendeleza mavazi ya Kitanzania na hatimaye Tanzania tuwe na vazi
moja rasmi la kujivunia wote.
5.
Kuendeleza fani ya mitindo na ubunifu
kwa kuwashirikisha wanamitindo, taasisi, mawakala na wabunifu wa Tanzania ili
kuiweka sanaa ya maonyesho ya mavazi katika thamani ya kimataifa.
6.
kutoa nafasi ya kutangaza na kuitangaza
nchi yetu ya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuhamasisha utalii.
7.
Kuwajengea Washiriki moyo wa kujitolea
ili waweze kutumia vipaji vyao katika kulitumikia Taifa kwa kujiajiri.
8.
Kujenga moyo wa mshikamano na Upendo
miongoni mwa Wanamitindo.
9. Kusaidia Jamii iliyo katika shida kutokana na
sehemu ya mapato yatakayo tokana mashindano haya.
10.
kuamsha ari ya Wasichana wa kitanzania
ili wajishughulishe na ujasiliamali na kujitegemea.
Wakati
wa kambi ya Tanzania Top Model, kutafanyika shughuli (Tasks)mbali mbali ambazo
zitaandaliwa na kufanywa na washiriki kama njia ya kujifunza, kupimwa uwezo wao
katika mambo mbali mbali(km uvumilivu, na kuburudisha watu watakao kuwa wanawaangalia
kwenye luninga . Tunaweza kusema kwa kifupi kuwa watu wasubirie Drama za
Washiriki watakaofanikiwa kuingia kwenye kambi ya Tanzania Top Model.
Mashindano
ya Mwaka huu yatahusisha nchi nzima lakini kwa kufanya usaili (auditions)
katika miji michache ambayo ni Dar es salaam (2), Mwanza, Musoma, Arusha,
Moshi, Dodoma, Mbeya na Iringa. Tutaendelea hivyo na kutakuwa na mabadiliko ya
kimfumo kila mwaka ili kuondoa uwezekano wa uchovu kwa washabiki wetu wa kuona
kitu hicho hicho kila mwaka.
Mshindi
wa shindano hili atapatikana baada ya kuonyesha kipaji chochote na kupata wastani
wa alama za juu kuliko wengine wane watakao kuwa wameingia kwenye fainali. Kwa
kufanikiwa kushinda, Tanzania Top Model atapata mkataba wa kufanya kazi na
Kampuni ya Tanzania Top Model Agency Ltd
kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo itakuwa ni pamoja na kushiriki
shindano la Top Model of the World. Wale
ambao hawatabahatika kushinda, wanaweza kupata mikataba ya ajira au ya
maonyesho mbali mbali kutokana na jinsi watakavyo kuwa wamefanya au kuonekana
kwenye vipindi vyetu vya Tamthilia halisi kwenye Televisheni.
Tunawahakikisha
wananchi kuwa hili litakuwa shindano litakalo wafundisha uvaaji wa mavazi
stahihiki kwenye maeneo husika na wakati gani na kwa wale tusiojua kuvaa tutakuwa
tumepata jukwaa la kutufundishia namna ya kuvaa na kuwa nadhifu muda wote
tukiwa wadau wa mavazi na mitindo.
Natanguliza
shukrani.
Jackson
M. Kalikumtima
Mwenyekiti
Mtendaji
No comments:
Post a Comment