Saturday, September 14, 2013

KAGERA SUGAR NA AZAM NGOMA DROO 1-1 UWANJA WA KAITABA, BUKOBA

Timu ya Kagera Sugar ndiyo iliyotangulia kupata bao kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kupitia mchezaji Themi Felix Buhaja aliyefunga bao la kichwa baada ya kupigwa kona katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 55 Khamis Mcha ‘Vialli’ aliisawazishia  Azam FC bao na kufanya mpira kuisha kwa matokeo hayo hayo mpaka dakika 90 za mchezo.
Katika mechi nyingine Coastal Union ilitoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mgambo Shooting kwa bao pekee la Elias Maguri dakika ya 53 Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani
 Oljoro JKT ilitoka sare ya 1-1  na Rhino Rangers Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, wenyeji wakilazimika kusawazisha dakika ya 27 kupitia kwa Amiri Hamad baada ya Saad Kipanga kutangulia kuwafungia wageni dakika ya tano, wakati Ashanti United ililala 1-0 mbele ya JKT Ruvu, 
Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam bao pekee la Amos Mgisa dakika ya 81. Matokeo hayo, yanamaanisha JKT Ruvu inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake tisa baada ya kushinda mechi zote tatu, ikifuatiwa na Simba SC katika nafasi ya pili yenye pointi saba. 
Timu nyingi zimefungana kwa pointi tano katika nafasi ya tatu, zikiwemo Yanga, Azam na Coastal Union.
Waamuzi wa Mtanange huu.
Picha ya pamoja
Waamuzi na timu kapteni wakijuzana kuhusu uelekeo wa kila timu
Kikosi kilichoanza cha Kagera Sugar
Bechi la Kagera pamoja na Viongozi wake.
Viongozi wa Kagera Suga kulia ni kocha mkuu.
Benchi la Azam Fc
Kipute kianze!!
Timu zote mbili zilianza kwa kukamiana! huku Azam FC wakijaribu kuingia kwenye eneo la Kagera Sugar mara kwa maraMchezaji wa Azam Fc akiondosha mpira kwa kichwa kuelekea goli la Kagera
Makocha wote wawili Azam Na Kagera Sugar wakiwajibika uwanjani hii leo

Kila mchezaji akitaka amchomoke mwenzake hapa!!
Mchezaji matata wa Azam Fc Kipre Cheche akimchomoka mchezaji wa Kagera Sugarr hapa na kuanza mbio za kasi!
Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Themi Felix baada ya kufunga bao dakika ya 25 baada ya kupigwa kona na yeye kumalizia kwa kichwa hadi nyavuni.
Wachezaji Kagera Sugar wakifurahia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.
Patashika!
Mchezaji wa Kagera Sugar akiondosha mbele mpira
Kocha wa Azam FC kulia akiangalia mtanange kipindi cha kwanza kuwa mgumu kwake!!
Mashabiki
Wadau mbalimbali wakitazama mtanange
Ilikuwa patashika hapa kwenye kipindi cha pili Timu ya Azam Fc ilipania kurudisha bao haraka iwezekanavyo na hatimaye kulipata baada ya dakika tano kupita!!
Khamis Mcha Vialli akishangilia baada ya kusawazisha bao dakika ya 55 kipindi cha pili.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia na kumpongeza mchezaji wao Mcha baada ya kusawazisha bao hilo
Angalia Viongozi wa Timu wanavyokuwa hapa, mwanzoni kocha wa Azam alilamika na kipindi hiki baada ya Kagera Sugar akaanza kuleta za kuleta !!
Kocha wa Azam Fc
Mpira umekwisha!!
Timu zote mbili zikitoka nje na sare ya bao 1-1.

No comments: